Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu wa Chama cha Kikoministi cha China kutoka Kamati ya Jimbo la Jiangsu Bw.Luo Zhijon,(kulia) akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni,[Picha na Ikulu.] 02/06/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu wa Chama cha Kikoministi cha China kutoka Kamati ya Jimbo la Jiangsu Bw.Luo Zhijon,(kulia) akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni,[Picha na Ikulu.] 02/06/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na Ujumbe wa Chama cha Kikoministi cha China kutoka Kamati ya Jimbo la Jiangsu ukiongozwa na Katibu wake Bw.Luo Zhijon,(kushoto) mara ujumbe huo ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni,[Picha na Ikulu.] 02/06/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na Ujumbe wa Chama cha Kikoministi cha China kutoka Kamati ya Jimbo la Jiangsu ukiongozwa na Katibu wake Bw.Luo Zhijon,(wa tatu kulia) mara ujumbe huo ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo jioni,[Picha na Ikulu.] 02/06/2016.
STATE HOUSE
ZANZIBAR
OFFICE OF THE
PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 2.06.2016
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
ametoa pongezi kwa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa kuendelea kuiunga
mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo ikiwemo sekta
ya afya.
Dk. Shein aliyasema hayo leo katika
mazungumzo kati yake na Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha China katika Kamati
ya Jimbo la Jiangsu Bwana Luo Zhijun akiwa amefuatana na ujumbe wake uliofika
Ikulu mjini Zanzibar.
Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alisema
kuwa azma ya Jimbo la Jiangsu kuendeleza mashirikiano yake kwa kuimarisha sekta
mbali mbali za maendeleo nchini ni hatua moja wapo ya kukuza uhusiano wa kidugu
uliopo kati ya pande mbili hizo.
Dk. Shein alipongeza azma ya Kiongozi
huyo katika kuimarisha uhusiano katika sekta ya afya, elimu, viwanda, uekezaji,
utalii pamoja uvuvi kati ya Zanzibar na Jimbo hilo la Jiangsu.
Aidha, Dk. Shein alieleza kuwa Zanzibar
itaweza kufaidika kwa kiasi kikubwa na makubaliano ya awali juu ya mafunzo kwa
madaktari na wauguzi wazalendo kati yake na Jimbo hilo, kwani ni hatua kubwa
katika kuhakikisha sekta ya afya inaimarika hapa nchini.
Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa
pongezi na shukurani kwa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kupitia Jimbo la
Jiangsu kwa utamaduni wa kuendelea kuwaleta
Madaktari bingwa kutoka Jimbo hilo tokea
mwaka 1964, ambapo mbali ya wataalamu hao pia, nchi hiyo imeweza kuleta wataalamu
wake mbali mbali hapa Zanzibar.
Aidha, Dk. Shein alitoa shukurani kwa
chama cha Kikomunisti cha China kwa kuendeleza ushirikiano wake na chama tawala
cha CCM na kuahidi kuendeleza mashirikiano hayo kwa kupanua wigo katika nyanja
mbali mbali za maendeleo.
Dk. Shein alisema kuwa ziara zinazofanywa
na viongozi wakuu wa vyama hivyo katika nchi mbili hizo zimeweza kuzidisha
mashirikiano makubwa yaliopo ambayo ni ya kihistoria.
Dk. Shein pia, alitumia fursa hiyo
kueleza uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya Jimbo hilo na Zanzibar na
kuahidi kuendelezwa na kudumishwa, huku akisisitiza kuwa China imeweza kutoa
mchango mkubwa katika mafanikio ya sekta mbali mbali hapa Zanzibar.
Pamoja na hayo, Dk. Shein alitoa pongezi
zake kwa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China chini ya kiongozi wake Rais Xie
Jingping kwa kuendelea kuisaidia na kuiunga mkono Zanzibar katika kuendeleza
miradi mbali mbali ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa Bandari, Hospitali ya Abdalla
Mzee Mkoani Pemba, Ujenzi wa Uwanja wa Mao tse Tung na ujenzi wa jengo jipya la
abiria katika uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
Nae Kiongozi huyo wa Jimbo la Jiangsu katika
maelezo yake, alieleza azma ya ziara yake hapa Zanzibar kuwa ni pamoja na
kusaini makubaliano ya awali ya mashirikino katika sekta ya afya baina ya
Hospitali za Jimbo hilo ikiwemo Hopitali ya Chuo Kikuu cha Nanjing na Hospitali
ya Mnazi MMoja.
Aidha, kiongozi huyo alisema kuwa ujio
wake una lengo la kusaidia vifaa vya tiba na madawa hasa katika matibabu ya akina
mama wajawazito na wanawake.
Kiongozi huyo alitumia fursa hiyo,
kumpongeza Dk. Shein pamoja na chama chake cha CCM kwa ushindi mkubwa uliopatikana
katika uchaguzi mkuu uliopita na kuahidi kuendelea kutoa mashirikiano kwa chama
hicho kwa lengo la kuendeleza udugu na mashirikiano yalioanzishwa na waasisi wa
mataifa hayo.
Sambamba na hayo, Kiongozi huyo alieleza
kuwa ushirikiano na uhusiano kati ya Zanzibar na China ni wa kihistoria ambapo
Jimbo la Jiangsu lilianza kutoa ushirikiano wake kwa kuleta madaktari hapa
Zanzibar tokea mwaka 1964.
Pamoja na hayo, Kiongozi huyo alimuahidi Dk.
Shein kuwa Jimbo lake litaimarisha ushirikiano katika sekta ya viwanda vikiwemo
viwanda vya nguo,
mashirikiano katika sekta za kiuchumi
hasa katika bidhaa za baharini, uvuvi pamoja na sekta ya utalii.
Pia, Kiongozi huyo alimuahidi Dk. Shein
kuwa mashirikiano zaidi yataimarishwa katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na utoaji
wa mafunzo kwa madaktari, wauguzi, mafunzo ya vyuo vya amali pamoja na ufundi.
Kwa upande wa sekta ya uwekezaji kiongozi
huyo alimuahidi Dk. Shein kuwa Jimbo lake litatoa mashirikiano zaidi katika
kuimarisha sekta ya uvuvi kwa kuanzisha viwanda vya uvuvi hasa kutokana na
Jimbo hilo kupata mafanikio makubwa katika sekta hiyo.
Pamoja na hayo, Kiongozi huyo alimueleza
Dk. Shein kuwa China inatoa nafasi nyingi za ufadhili wa masomo hivyo
alisisitiza haja kwa Wazanzibari kujiunga na vyuo vikuu vilivyomo Jimbo hilo.
Kiongozi huyo pia, alisisitiza haja ya
kuimarisha mashirikiano na uhusiano uliipo kati ya Jamhuri ya Watu wa China na
Tanzania ikiwemo Zanzibar.
Rajab Mkasaba,
Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment