Habari za Punde

Wanachama ‘tufaane’ wakopa 239 milin


Na Haji Nassor, Pemba
WANACHAMA 135 wa ushirika wa ‘tufaane saving and credit’ wa wizara ya ardhi, makaazi, maji na nishati Pemba, wameshakopesha mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 239, hadi kufikia mwezi disemba mwaka 2014 kwa wanachama wake.
Kati ya fedha hizo shilingi milioni 122.5 tayari zimesharejeshwa na wakopaji, wakati shilingi milioni 150.3 bado ziko mikononi mwa wanachama, wakiendelea kurejesha taratibu.
Akisoma risala ya ushirika huo, kwenye mkutano mkuu uliofanyika ofisi ya mamlaka ya maji ‘ZAWA’ Machomane Chakechake, Katibu Khamis Hamad Hassan, alisema hayo ni miongoni mwa matunda ya uhsirika wao.
Alieleza kuwa, pia ushirika umefanikiwa kukopesha shilingi zaidi ya milioni 6.5 kama mikopo ya dharura na shilingi milioni 143.8 mikopo ya kawaida miongoni mwa wanachama.
Katib huyo alifafanua kuwa, iwapo wanachama waliochukua mikopo hiyo wameekeza kwenye mitaji mbali mbali, itakuwa wameshapiga hatua ya kimaendeleo.
“Ushirika wetu umefikia pahala pazuri, maana wapo wanachama 135 hadi kufikia mwaka juzi, wameshachukua mikopo, na ndio miongoni mwa malengo yetu’’,alifafanua.


Akifungua mkutano huo Katibu tawala wilaya ya Chakechake Abdalla Rashid Abdalla, aliwashauri wanachama hao kuwa makini wanapochukua mikopo, ili faida ya kukopa kwao ionekane.
Alieleza kuwa, wapo wanachama katika vyama vyengine vya ushirika, wamekuwa wakikopa fedha na kisha kujinunulia chakula badala kuanzisha mitaji yenye thamani.
Katika hatua nyengine Katibu huyo tawala amewasisitiza wanachama wa ushirika huo, kuendelea kutoa michango na ada zao, wakiamini kwa njia hiyo inaweza kukuza ushirika wao.
Afisa ushirika Yussuf Seif Yussuf, alisema lazima uongozi wa ushirika huo, ujiwekee malengo ya kutoa mikopo mikubwa kwa njia ya kuongeza hisi za wanachama.
Mshika fedha wa ushirika huo Juma Ali Juma, alisema kiujumla ushirika huo, umepiga hatua ya kimaendeleo na ndio maana, umefikia kutoa hadi mikopo yenye thamani ya shilingi zaidi ya milioni 239.

Ushirika wa ‘tufaane saving and credit’ ambao umeanzishwa mwaka 1992, ukiwa na waanchama 45 na sasa ukiwa na wanchama 201, bado unaendelea kukumbwa na changamoto ya uhaba wa mitaji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.