Habari za Punde

Ziara ya Waziri wa Ujenzi Balozi Ali Karume Kisiwani Pemba.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano, Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar Mhe: Balozi Ali Abeid Karume, akiwa na baadhi ya watendaji wa wizara yake, wakielekea kwenye ujenzi wa ukuta maalumu, kwa ajili ya kuzuia eneo la barabara ya Bahanasa- Mtambwe isikatike
Aliyekuwa Mhandisi wa ujenzi wa barabara sita za mkoa wa kaskazini Pemba, zilizojengwa na Kampuni ya H-Young Japhet Malambi, akimpa maelezo Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano, Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar Mhe: Balozi Ali Abeid Karume, alipokuwa akikagua ujenzi wa ukuta maalum kwa ajili ya kuzuilia eneo la barabara ya Mtambwe isikatike
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano, na Usafirishaji Zanzibar Mhe: Balozi Ali Abeid Karume, akifafanua jambo, kwenye eneo la ujenzi wa ukuta maalumu kwa ajili ya kuzuia barabara ya Bahanasa- Mtambwe isikatike, wakati waziri huyo na ujumbe wake, ulipofika eneo hilo kukagua barabara kisiwani Pemba.
Afisa Mdhamini Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Pemba, Hamad Ahmed Baucha (wa tatu kulia), akimuonyesha ramani Waziri Balozi Ali Abeid Karume (wa pili kulia) na Katibu Mkuu Mustafa Aboud Jumbe (mwenye kofia) na Naibu Waziri Mhe: Mohamed Ahmad Salum (kushoto), wakati viongozi hao walipokuwa kisiwani Pemba kwa ziara ya siku mbili,
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe: Balozi Ali Abeid Karume, akiwa na baadhi ya watendaji wa wizara yake, wakikagua nyumba za maendeleo zilizopo Wete Pemba, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili kisiwani Pemba
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe: Balozi Ali Abeid Karume, akiwa na baadhi ya watendaji wa wizara yake, wakikagua nyumba za maendeleo zilizopo Wete Pemba, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili kisiwani Pemba
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe: Balozi Ali Abeid Karume, akiangalia nyumba zilizochakaa za maendeleo zilizopo Mtemani Wete, nyuma yake ni Mdhamini wa shirika la nyumba Pemba Suleiman Hamad Omar
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano, Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar Mhe: Balozi Ali Abeid Karume (wa nne kulia) akiwa na baadhi ya watendaji wa shirika la bandari, wakikagua bandari yaWete kisiwani Pemba, wakati waziri huyo alipokuwa na ziara ya siku mbili kisiwani humo.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe: Balozi Ali Abeid Karume, akiwa na mwanasheria wake Rashid Juma Mohamed, wakiteta jambo kwenye eneo la barabara ya Mgagadu- Kiwani wilaya ya Mkoani, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili kisiwani humo.
 (Picha na Haji Nassor, Pemba).

1 comment:

  1. Post habari ya jana baraza la wakilishi tafadhali

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.