Habari za Punde

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, Mhe. Haji Omar Kheri Akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, Mhe. Haji Omar Kheri akiwasilisha hutuba ya Wizara yake katika Mkutano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, kwa wajumbe wa baraza kuchangia na kupitisha bajeti za wizara za serikali.  
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia Hutuba ya Bajeti ya Wizara hiyo.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe Simai Mohammed Said akiwa katika ukumbi wa mkutano akifuatilia hutuba hiyo.
Wajumbe wakifuatilia hutuba hiyo wakati ikiwasilishwa katika Mkutano wa Baraza la Wawakilishi. Mhe Juma Ali Khatib akifuatilia hutuba ya Bajeti ya Wizara ya Tawala za Mikoa  wakati ikiwasilishwa katika Mkutano wa Baraza jana.
Wajumbe wakifuatilia Hutuba ya Bajeti wakati ikiwasilishwa na Waziri husika Mhe Haji Omar Kheri.
Maofisa wa Idara za Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala wakiwa nje ya Ukumbi wa Mkutano baada ya kuahirishwa jana kwa mapumziko ya asubuhi.
Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Pemba akizungumza na Wajumbe wa Baraza wakati wa mapumziko ya mchana baada ya kuchangiwa Bajeti ya Wizara hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, Mhe. Haji Omar Kheri, akizungumza na watendaji wa Wizara yake baada kuahirishwa kwa baraza kwa mapumziko ya mchana jana.
Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum Mhe Said Soud Said akizungumza na Mwakilishi wa Jimbo la Chukwani Zanzibar Mhe Mwanaasha Khamis Juma, wakati wa mapumziko ya mchana baada ya kuwasilishwa hutuba ya Bajeti ya Wizara Nchi Ofisi Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ. Jana

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.