Habari za Punde

Jumuiya ya Shia Wamkabidhi Madawati Rais wa Zanzibar Dk.Shein

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya  Khoja Shia Ithna-asheir Mhe,Mohamed Raza Daramsi wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akifuatana na Viongozi na Mashekhe wa jumuiya hiyo kwa ajili ya kukabidhi msaada wa madawati 100 kwa  ushirikiano na familia ya Rais wa Jumuiya,msaada huo utaowanufaisha wanafunzi wa Skuli mbali mbali za Zanzibar
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma akitoa shukurani kwa Uongozi wa Jumuiya ya  Khoja Shia Ithna-asheir wakati ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kukabidhi madawati 100 kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) ikiwa ni katika kuimarisha sekta ya Elimu hapa Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipokea zawadi maalum kutoka kwa  Mashekhe wa Jumuiya ya  Khoja Shia Ithna-asheir (kulia) Sheikh Shaaban Hussein,Sheikh Maulana Dhishan  Haidar  na Rais wa Jumuiya hiyo Mhe, Mohamed Raza (kushoto) wakati walipofika ikulu Mjini Zanzibar kukabidhi msaada wa madawati 100 kawanafunzi wa Zanzibar
Rais wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir Mhe,Raza (kushoto) akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia aliyekaa) wakati Jumuiya hiyo ilipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kukabidhi madawati 100 kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar ikiwa ni katika katua za kuimarisha sekta ya Elimu nchini
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia)akikabidhiwa madawati 100 kutoka kwa Viongozi wa jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir na familia ya Rais wa Jumuiya hiyo Mohamed Raza walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,msaada huo  kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar, 02/07/2016.[Picha na Ikulu.] 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.