Umati wa wakazi wa jiji na New York waliojitokeza katika tamasha hilo fedha zinazopatikana kupitia tamasha hilo hupelekwa kusaidia masuala mbalimbali ya kijamii. Tamasha hilo lilitumbuizwa na wanamziki maafuru akiwamo Rihanna ambaye ametangazwa kuwa Balozi wa Elimu.
Rais Mstafu Jakaya Kikwete, na Kamishna wa Kamisheni ya Kimataifa kuhusu elimu akizungumza mbele ya umati wa wakazi wa jiji la New York katika tamasha la Global Citizen Festival lililofanyika Central Park. Kupitia tamasha hilo, Kikwete aliichagiza jumuiya ya kimataifa kuchangia na kuwekeza katika elimu kwa mustakabali wa kizazi cha sasa na kijacho. Pamoja naye ni Makamishna wenzie, Waziri Mkuu wa Norway Erna Solberg na aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Australia Julia Gillad.
Rais Mstaafu Kikwete akisalimiana na Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Samantha Power walipokutana kwenye tamasha hilo.
Na Mwandishi
Maalum,New York
Rais Mstaafu
wa Tanzania, Jakaya Mrisho
Kikwete, amasema, Afrika itandelea
kubaki nyuma kielimu ikiwa jitihada za makusudi hazitafanyika kuwekeza katika elimu.
Ametoa kauli hiyo jana jumamosi
mbele ya maelfu kwa mamia ya wakazi wa
Jijini la New York waliofurika Central Park kuhudhuria tamasha
maarufu lijulikanalo kama Global Citizen Festival.
Tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka huwaleta pamoja viongozi
kwa kada mbalimbali, wanaharakati na idadi kubwa
ya waungaji mkono wa juhudi za kuutokomeza umaskini uliokidhiri
na limeandalia na mtandao
wa Uraia wa Kimataifa ( Global
Citizen) kwa pamoja na
Ushirikiano wa Kimataifa kuhusu
Elimu ( Global Partnership for Education)
.
Aidha fedha zinazopatika kupitia tamasha hilo
hutumika katika kusaidia masuala
ya kimandeleo kama yakiwamo ya
afya, elimu, mazingira, usalama wa chakula pamoja na masuala yanayohusu wanawake na watoto wa kike.
Ni katika
tamasha hilo ambalo mwaka huu limelenga pamoja na
masuala mengine, fursa ya elimu kwa watoto wote
ambapo, Rais Mstaafu Kikwete ambaye pia ni Kamishna katika
Kamisheni ya Kimataifa kuhusu Elimu, ameitaka
jumuiya ya kimataifa kupitia
hadhara hiyo kusaidia na kuwekeza katika
eneo hilo muhimu kwa mustakabali wa
kizazi cha sasa na kijacho.
“ Afrika yangu, itakuwa makazi ya vijana bilioni moja
ifikapo mwaka 2050, na tayari ipo nyuma
kielimu” akasema Kikwete na kuongeza. “Kama
hatutawawezesha vijana wote sasa
kwa kuwapatia ujuzi na maarifa , uchumi utapoteza kiasi cha dola 1.8 trilioni na watoto 800 milioni
hawata kuwa shuleni ifikapo mwaka 2030. Na hii ni gharama ya kutoelimisha sasa”
Rais Mstaafu aliyezungumza na
halaiki hiyo kwa pamoja na Makamishna
wenzie, Waziri Mkuu wa Norway Bi. Erna
Solberg na Waziri
Mkuu wa zamani wa Australia, Bi. Julia Gillard ambaye ni pia ni Mwenyekiti wa Ushirikiano wa Kimataifaka kuhusu Elimu (
GPE).Amesisitiza kwamba “ Ni lazima tujenge kizazi kinachojifunza kwa
kuogeza fedha kiasi cha dola 3 trilioni ifikapo mwaka 2030. Washirika wa maendeleo ni lazima waungane nasi katika misheni yetu hii,
na sehemu kubwa ya fedha lazima zitoke katika vyanzo
vya mapato vya ndani”.
Katika harakati hizo za
kuwafikishia fursa ya elimu watoto wote wa kike na
kiume, Global Partnership for Education and Global Citizen, wamemtangaza mwanamziki maarufu wa Marekani Rihanna kuwa Balozi wa
Elimu ambapo kupitia
Taasisi yake ya Clara Lionel watafanya kampeni ya pamoja na
Global Partinship for education na Global Citizen kuhakikisha
kwamba watoto wote wa kike na wa kiume wanapa fursa ya elimu bora.
Jukumu jingine la mwanamziki huyo
ni pamoja na kuwahamasisha viongozi wa
dunia kuunga mkono uwekezaji katika elimu nchini mwao.
Rihanna na wanamuziki wengine maarufu alitumbuiza
katika tamasha hilo.
No comments:
Post a Comment