Habari za Punde

Innaa Lillahi wa Innaa Ilayhi Raajiun. Mzee Mussa Haji Foum Mwandishi Muandamizi Zanzibar Afariki Dunia jana kwa Kugongwa na Gari Maeneo ya Rahaleo Zanzibar.

Muandishi wa Habari wa siku nyingi Zanzibar aliyekuwa akifanyia kazi Sauti ya Tanzania Zanzibar kwa sasa ZBC Redio Marehemu Mussa Haji Foum amefariki dunia jana kwa kugongwa na gari katika eneo la rahaleo Unguja wakati akivuka barabara akitokea Masjid Mushawar kusali sala ya magharibi na kumkuta mauti hayo jana jioni katika eneo hilo. 

Gari iliomgonga ilikimbia baada ya kuona imetenda kosa hilo. 

Marehemu alikimbizwa hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kwa matibabu na kufariki alfajiri ya leo na kuzikwa kijiji kwao Mwache alale Kikombetele, Mkoa wa Kusini Unguja saa saba mchana. Mwenyenzi Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu Ameen.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.