MUONEKANO
MPYA WA TOVUTI YA ZSSF.
Mfuko
wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) ambao ni mfuko
pekee wa hifadhi ya jamii
Zanzibar, unapenda kuwataarifu
wanachama
wake na jamii kwa ujumla kwamba, kutokana na
mabadiliko ya kiteknolojia na
mahitaji ya wanachama wake
imeboresha huduma zake kwa sasa kupitia Tovuti yake.
Tovuti hiyo
ya ZSSF, www.zssf.org ilikuwa ikifanyiwa marekebisho makubwa miezi
michache iliyopita ili kuweza kukidhi mahitaji ya wanachama wake na kuondosha kasoro zilizopo. Kwa sasa kupitia Tovuti ya ZSSF ambayo pia imeunganishwa na mitandao mengine ya kijamii ikiwemo face
book, inawawezesha wanachama wake kufanya usajili, kuona michango yao na
kuuliza maswali popote walipo. Pia wanaweza
kutoa malalamiko au mapendekezo yeyote kuhusiana na ZSSF.
Kutokana na maboresho
hayo, wanachama wanaweza kujua zaidi
kuhusiana na Mfuko unaojumuisha Mfuko Mkuu ambao ni lazima
kwa
kila muajiriwa kujiunga na Upo Mfuko wa Hiari (ZVSSS)
kwa Wajasiriamali na Mtu yeyote anaweza kujiunga nao.
Aidha tovuti hiyo
inatoa taarifa za Miradi na Uwekezaji wa Mfuko
kama vile Maduka ya
Mwanakwerekwe , Mnara wa Kumbukumbu
ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar, Viwanja vya Kariakoo ,
Tibirinzi
pamoja na habari na matukio ya Mfuko kwa
jamii.
Mfuko wa Hifadhi ya
jamii Zanzibar unapenda kuwahakikishia wanachama wake na jamii
kwa ujumla kwamba ,Tovuti yake
itaendelea kuwa na muonekano mpya kadri siku zinavyoendelea kupitia huduma
zake. Pia inawaomba wanachama na wasiokuwa wanachama kutembelea Tovuti hiyo ili kuhabarika na kuuliza
masuali na kutoa maoni yao kwa lengo la kuimarisha Mfuko wa ZSSF.
Imetolewa na :
Kitengo cha Masoko na Uhusiano.
MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR
MAKAO MAKUU KILIMANI MNARA WA MBAO. S.L.P 2716
SIMU:+255-24
2230242, FAKSI:+255242232820,
Barua pepe:info@zssf., Tovuti.www.zssf.org.
“ZSSF
NI UFUNGUO WA MAISHA YA BAADAE”
###
No comments:
Post a Comment