Assalaamu Alaykum warahmatu Llaahi wabarakaatuh
Ndugu waislamu.
Sisi ni walimu wa madrasa ya Qur-an iliopo Kilimani Zanzibar.
Kutokana na kukua kwa harakati zetu katika madrasa yetu
مدرسة النهضة الإسلامية
Madrasatun Nahdhatul Islamiya
Jengo letu tunalotumia sasa kusomeshea watoto limekua halikidhi tena haja, ni dogo mno.
Hivyo kwa kipindi kirefu sasa madrasa yetu imekua ikitafuta eneo jengine ili kukuza harakati zake za kuwalea watoto wetu wa kiislamu na kuwapa elimu ya dini yao, sambamba na kuwafundisha tabia zilizo njema.
Na kwa tawfiq yake Allah Subhaanahu Wata'ala tayari eneo hilo limepatikana tena uzuri zaidi lipo hapa hapa Kilimani makao makuu ya harakati zetu.
Wamiliki wa eneo hilo wanaliuza Tsh milioni sitini za kitanzania Sh 60,000,000/=, na Madrasa imelizuia lisiuzwe kwa mtu mwengine bali tusubiriwe sisi tulinunue.
Na muda tuliopewa kwa kweli unaelekea kumalizika na hadi sasa mbio zetu tumeza kukusanya milioni kumi na tisa tu sh 19,000,000/= pesa taslim.
Na ahadi za watu mbali mbali kwa sasa zinafikia milioni kumi na mbili.
Hivyo basi kutokana na hali ya Madrasa kua ni ngumu na uwezo huo kwa sasa hatuna, lakini kwa kua hili ni jambo la kidini tumesema tusivunjike moyo wala tusirudi nyuma na tunaamini kwa kushirikiana na waisilamu wenzetu tunataraji hili halitotushinda inshaallah.
Tunapokea michango yenu katika hili, kila mmoja atoe alichonacho kwa kadri ya hali yake na uwezo wake wa kimali alioruzukiwa na Allah, na Allah anatuona na anazijua hali zetu dhahiri yetu na siri yetu.
Na chochote utakachotoa katika hili na ukatia nia nzuri katu hakitopotea bali mbele ya Allaah ni kikubwa na chenye malipo mazuri kabisa.
Tunapokea kuanzia Tsh mia tano tu ya kitanzania sh 500/= basi usikubali kupitwa na kheri hii adhimu kwani sote tunao uwezo huo na zaidi ya hapo.
Na kama unamjua mtu anaeweza kutoa msaada wake katika hili TUNAKUOMBA UZUNGUMZE NAE umfahamishe vizuri ili utusogezee na utuunganishe nae inshaallah, Mtume (S.A.W) anasema:
الدال على الخير كفاعله
(Mwenye kujuulisha jambo la kheri hupata malipo sawa na alielifanya)
Kwa maelezo zaidi piga simu:
Uongozi wa Madrasa:
+255 24 2235913
Mwalimu Mkuu:
+255 773 092 153
Msajili wa Madrasa:
+255 772 337 913
Shiriki kuueneza ujumbe huu.
Ahsanteni sana.
No comments:
Post a Comment