Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mhe Sadifa Juma leo ameongoza ujumbe wa viongozi wa UVCCM kumfariji na kumpa pole msanii wa maigizo ndg Abdul Ahmad jina la Usanii Ben Serengo nyumban kwao Kigogo Jijini Dar Es Salam, aliyepata ajali ya gari tareh 25 siku ya skukuu ya Christmas.
UVCCM inathamini sana mchango wa wasanii wa ndani na inaguswa na changamoto na matatizo mbali mbali yanayopata wasanii hivyo Jumuiya itaendelea kuwa nao karibu kwa kuzingatia umuhimu wao katika jamii na Chama Cha Mapinduzi. Alisema Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mhe:Sadifa Juma Khamisi(MCC/MB) alipokwenda Kumjulia Hali Msanii wa Bongo Movie Abdul Ahmad jina maarufu Ben Serengo wa pili kulia na wa tatu kulia ni Kaimu katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Sadifa Juma Khamisi(MCC/MB) wa nne kulia akitizama picha mbali mbali za tukio la ajali Msanii wa Bongo Movie Abdul Ahmad jina maarufu Ben Serengo wa Tatu kulia iliyotokea tareh 25 Siku ya Skukuu yaChristmas.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Sadifa Juma Khamisi(MCC/MB) wa Tatu kushoto akizungumza na mama wa msanii Bi Jasmin Rajabu Hatia Mara baada ya kutoka kumuona mgonjwa.
No comments:
Post a Comment