Habari za Punde

Rais Dk Shein awaapisha viongozi aliowateua Karibuni Ikulu



STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
  Zanzibar                                   6.2.2017
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  leo amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni kushika nyadhifa mbali mbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Viongozi walioapishwa ni Ibrahim Mzee Ibrahim kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Jaji Rabia Hussein Mohamed kuwa Mwenyekiti wa Mahkama ya Rufaa ya Idara Maalum za SMZ, Asha Ali Abdalla ambaye anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Wengine ni  Yakout Hassan Yakout ambaye anakuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Seif Shaaban Mwinyi ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora anayeshughulikia Utumishi wa Umma.

Hafla hiyo, ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Jaji Mkuu wa Zanzibar  Omar Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji.

Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud,  Wakuu wa Vikosi vya SMZ, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.