Habari za Punde

Serikali Kuchimba Mabwawa ya Maji Ili Kupunguza Uhaba wa Maji Nchini.

Na Husna Saidi.Maelezo Dar es Salaam.                                                                           

SERIKALI imesema imeandaa mpango kabambe wa uchimbaji wa mabwawa ya kutiririsha maji ya mvua katika baadhi ya maeneo nchini ili kupunguza hadha ya ukosefu wa maji kwa wananchi.

Hayo yamebainishwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo na Wazirti katika kikao cha Bunge la bajeti linaloendelea Mjini Dodoma.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema katika kutekekeleza mpango wa Serikali kumtua “Mama ndoo kichwani” Serikali imedhamiria kupunguza umbali mrefu wanaotumia wananchi kutafuta maji, ambapo imepanga kuchimba mabwawa makubwa ya maji katika  maeneo ambayo yana mtiririko wa maji.

“Tutaendelea kutoa maelekezo kwa Watendaji wetu kuhamasisha wananchi kutumia fursa ya misimu wa mvua ili kujiwekea akiba ya maji ambayo yatawasaidia wakati wa kipindi cha kiangazi hususani katika maeneo ambayo yana uhaba wa maji”.

Kwa mujibu wa Majaliwa alisema katika Bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Serikali imeandaa mpango maalum wa uchimbaji wa mabwawa ya maji sambamba na kufanya ukarabati wa mabwawa ambayo yameharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa alizitaka Halamashauri zote nchini kuhakikisha zinatumika vyema mabwawa na mifereji iliyokuwa katika maeneo ili kuweza kuvuna maji ya mvua na kuyahifadhi kwa msimu huu wa mvua na ujao.

Majaliwa aliongeza kuwa Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya mabwawa yote nchini ili kuhakikisha halmashauri zote nchini zinakuwa na utoshelevu wa huduma ya maji kwa wananchi wake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.