Habari za Punde

Mchezo wa Kirafiki wa Timu ya Jangombe Boys na Gulioni Kufanyika Kesho Amaan Usiku.Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Timu ya Gulioni FC bado inaendelea na mchakato wake wa kujiweka sawa kucheza ligi Daraja la Kwanza Taifa Unguja msimu mpya ambapo kesho Alhamis Iddi nne watacheza mchezo mwengine wa kirafiki na timu ya Jang’ombe boys, mchezo ambao utasukumwa saa 2:00 za usiku katika Uwanja wa Amaan.

Gulioni jana walipigwa 2-1 na Taifa ya Jang’ombe katika mchezo wa kirafiki ambapo kesho wamepania kufuta makosa yao mbele ya Boys.

Viingilio vya mchezo huo ni Shilingi 2000/=, 3000/= na  VIP 5000/= .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.