Habari za Punde

Zanzibar kuanza kutumia risiti za kielektroniki

ALI Issa Na Kijakazi Abdalla Maelezo   29/6/2017

Imeelezwa kuwa Mashine mpya za kisasa za kielectronic za utoaji wa risiti baada ya mauzo kwa wafanya biashara itasaidia kuondoa  udanganyifu katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kumpa uhalali mteja wa kile alicho kinunua.

Hayo yamesemwa leo huko ZRB mazizini Zanzibar katika ofisi ya mamlaka hiyo ya ukusanyaji mapato zanzibar na kamishina wa bodi ya mapato   Amuor Hamili Bakari wakati akifungua semina kwa wandishi wa habari .

Amesema kumekuwa  na utata wa  muda mrefu kwa wafanya biashara juu ya suala zima la kutoa risiti kwa wateja na kupelekea ukusanyaji wa mapato kukusanya mapato yasio na uhakika kwa walicho kikusanya kwa watu hao jambo ambalo huleta masikitiko kwa madai kuwa hawajauza na wanatozwa kodi kitu ambacho si kweli.

Amesema mashine hizo mpya zitaeleza ukweli juu ya wafanyabiashara alichokiuza kwani kumbukumbu zote zitakuwa zina onekana bila kuwa na ubabaishaji kwa mauzo yake.

“tumebaini kuwa wafanya biashara wengi hawalipi kodi lakini tutapo wakabidhi mashine hizi tutajuwa ukweli wa kile alicho kikusanya na kodi yake ikoje.”alisema Amour.

Aidha aliitaja mashine hiyo kwajina  (EFD) Electronic fisical devis ambazo zinatarajiwa kufanya kazi kwa awamu ya kwanza mwezi wa Novemba mwaka huu ambapo wafanyabiashara wataowahi kupata mwazo watapewa bure bila ya malipo. 

Nae meneja sera utafiti na mipango Ahmed Haji Sadat alipokuwa akiwasilisha mada ya matumizi ya elektronic alisema kuwa mfanya biasha kutoa risiti ni suala la kisheria na hapaswi kupinga kutoa risiti na itapo bainika mfanya biasha hakutoa risiti atachukuliwa hatua za kisheria


  Amesema kuwa malipo hayo yatalazimika kwa kila mtu wakiwemo hata wageni  ambapo kutakuwa na mfumo maalum kwa ajili ya waingizaji wageni wanaoingia na kutoka nchini.

Pia ameelezea lengo la risiti hizo ni kupatikana mapato ya serikali kwa ufanisi ambapo wananchi waelimishwe kutumia risiti hizo ambapo taasisi mbali mbali zote zitapaswa kutumia risiti hizo.

Meneja huyo amesema taarifa zote zitakuwa kwenye usalama mkubwa na haziwezi kupoteana zitaweza kutuma ripoti baada ya manunuzi kwa mnunuzi na mfanyabiashara.

Aidha amesema endapo mfanyabiashara wa aina yeyote hatotowa risiti kw mnunuzi sheria kali zitachukuliwa dhidi yake iwapo atapobainika akitenda kosa hilo.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.