Habari za Punde

Masheha na Madiwani Wapata Elimu ya Sheria ya Ugatuzi wa Madaraka

Mkuu wa wilaya ya Micheweni Pemba, Abeid Juma Ali akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria, kwa masheha na madiwani wa Mkoa wa kaskazini Pemba, yalioandaliwa na kufanyika Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, kulia ni Mratibu wa kituo hicho Fatma Khamis Hemed, na kushoto na mratibu wa mafunzo hayo, Safia Saleh Sultan
Masheha na madiwani kutoka Mkoa wa kaskazini Pemba, wakifuatiliaji utaoji wa mada kadhaa, kwenye mafunzo ya kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria, mafunzo yalioandaliwa na kufanyika Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ tawi la Pemba
Mtoa mada ya Ugatuzi wa madaraka Said Makame Said, akiwaelezea masheha na madiwani wa Mkoa wa kaskazini Pemba, kwenye mafunzo ya kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria, yaliofanyika Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ tawi la Pemba
Mtoa mada ya haki za binadamu, mwanasheria Safia Saleh Sultan, kwenye mafunzo ya kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria, kwa masheha na madiwani wa wilaya za Micheweni na Wete mkoa wa kaskazini Pemaba, yaliofanyika ofisi ya ‘ZLSC’ mjini Chakechake.
Sheha wa shehia ya Micheweni Dawa Juma Mshindo akiomba ufafanuzi wa maana ya neno wasaidizi wa sheria, kwenye mafunzo yaliowashirikisha masheha na madiwani wa Mkoa wa kaskazini Pemba, yenye lengo la kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria, yaliofanyika Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ tawi la Pemba.
 (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.