Habari za Punde

Nafasi za kazi Wizara ya Ardhi,Maji, Nishati na Mazingira

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira kama ifuatavyo:-

1. Afisa Mipango Miji Daraja la II “Nafasi 3”

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya Mipango Miji kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Mchumi Daraja la II “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Uchumi’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Afisa Ardhi Daraja la II “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya Usimamizi Ardhi na Uthamini kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4. Mchoraji Ramani Daraja la III “Nafasi 2”

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya ‘Stashahada’ katika fani ya ‘Catographer’ au ‘Civil Engineer kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5. Mtunza Ramani Daraja la III “Nafasi 2”

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari
• Awe amehitimu elimu ya ‘Stashahada’ ya ‘Kumbukumbu’ au ‘Geography’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

6. Mkaguzi Eka Daraja la III “Nafasi 2”

Sifa za Waombaji:

• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya ‘Stashahada ya Kilimo’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

7. Afisa Tehama Daraja la II “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Teknolojia ya Habari’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jinsi ya Kuomba:

• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-

a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.

f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 21 Julai, 2017 wakati wa saa za kazi.

1 comment:

  1. Mr Othman mm hupenda sana post zako, lkn nahisi sometimes huwa unatufanyia mzaha, sijui ndiyo unavyozipata hizi habari ama vipi au ndo uhalisia wenyewe. Tangszo la nafasi za kazi umetuletea leo 8:40AM 20 JULY 2017, DEAD line ya kuwasilisha maombi ni 21 July 2017 how come shk wangu. Kulikoni hebu tupe sababu, au ndo hali halisi ilivyo wanaotakiwa kwenye hizo nafasi wadhapatika, iliyobaki ni kuzuga watu tu?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.