Habari za Punde

Mswada kuanzishwa bima ya afya kazini upo jikoni, tayari umeshapitishwa na makatibu wakuu wa serikali

Na Ali Issa                                        Maelezo                         

Mswada wa  sheria ya kuanzisha Bima ya afya kazini kwa watumishi wa Umma  Zanzibar tayari umepitishwa kwenye kamati ya makatibu wakuu na baraza la Mapinduzi zanzibar .

Hayo yamesemwa leo huko baraza la wawakilishi nje kidogo ya mji wa Zanzibar katika kikao kinacho endelea na waziri wakazi,uwezeshaji,wazee  ,vijana,wanawake na watoto Moudline Cyrus Castico wakati akijibu maswali ya Ripoti ya ufafanuzi wa ushauri uliotolewa na kamati ya maendeleo ya wanawake, habari  na utalii ya Baraza la wawakilishi.

 Amesema mswada huwo wa Sheria  wa kuanzishwa bima hiyo kwa wafanya kazi wa umma sasa hivi upo katika ofisi ya mwanasheria mkuu wa Zanzibar kufanyiwa marekebisho yanayo stahiki na hatimae utawasilishwa  baraza la wawakilishi.

Amesema hatua imekuja badayakuona kuwa wafanya kazi wanafanya kazi muda mwingi na kupatwa na matatizo mbali mbali ya kiafya jamboamalo kwa ghafla wafanya kazi hushindwa kujitibu hivyo bima hiyo kwa wajiriwa ni muafaka kwao kwani  itawasaidia kujitibu maradhi, majanga ya ajali kazini na kupata matibabu ya uhakika pale tokeo limetokea.

Amsema hali hiyo itawasaidia wafanyakazi kuona kuwa wanajaliwa na watumishi wao kwani wao ni watumishi na waleta wamaendeleo kwa Taifa lao.

Akizingatia ushauri huo wa ripoti hiyo  suala la afya ya usalama kazini waziri huyo alisema wizara kupitia idara ya usalama na afya kazini idara inaendelea kufanya ukaguzi kwenye sehemu za kazi ili kuona wafanya kazi wanafanya kazi katika hali ya usalama na kupatiwa vifaa vya kinga kulingana na kazi yake.

Alisema katika kusimamia suala hilo kwa ufanisi,idara imetayarisha rasimu za kanuni zitakazo wabana wajiri na wajiriwa kutekeleza suala hilo kwa mujibu wa kifungu cha sheria 116(1) na (2) cha sheria ya usalama na afya kazini namba 8ya mwaka 2005.

 Hata hivyo alisema wizara imefanya ukaguzi wa usalama kazini mwaka 2016-17katika taasisi 139  kwa unguja na pemba.

Alitaja maeneo walipita ni pamoja na viwanda ,taasisi za ujenzi mahoteli na vituo vya mafuta,ambapo kila tassisi ilielezwa vifaa vya kununua kwa ajili ya kuwakinga wafanyakaziwao kwa mujibu wa kazi wanazo fanya.

Wakati huohuo waziri huyo aliwahidi vijana wale wote wa Zanzibar waliopo katika mabaraza ya vijana wanao hitaji mikopo na wanao kidhi vigezo vinavyo hitajika watapatiwa mikopo bila ya usumbufu wowote.

Amesema kutokana na uzowefu walio nao katika mfuko wa uwezeshaji wananchi kiuchumi ,unaosimamiwa na wizarayake hilo linawezekana kwa wale waliopo katika mabaraza.

1 comment:

  1. mshaurini Waziri apite ZANZIBAR AIRPORT aone wale Security wanaovyokufa na MIONZI (Radiation) za zile mashine ...wakiishi ktk mzingira magumu bila ya kuthaminiwa wala Kugaiwa posho yoyote ile km MAZIWA na posho la mazingira hatarishi ...hapo ndo usalama kazini.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.