Mkurugenzi wa Kampuni ya Pannyroyal Zanzibar Amber Resort Saleh Mohammed Said akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ufadhili wa kampuni yao kwa shughuli za Kijamii katika Kijiji cha Matemwe Mkoa wa Kusini Unguja, wakati wa mchezo wa ligi daraja la pili wilaya ya kaskazini unguja Mradi wa Zanzibar Amber Resort, inafadhili timu za Kijiji cha Matemwe.
MKUU
wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Vuai Mwinyi akiikagua timu ya Amber Sports Club
inayofadhiliwa na kampuni ya Pennyroyal katika mchezo wa ligi ya soka daraja la
tatu Wilaya ya Kaskazini ‘A’ kati ya timu hiyo na Kijini Stars zote za Matemwe,
katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa New Stars Mkwajuni
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Vuai Mwinyi akiikagua timu ya Kijini Stars
katika mchezo wa ligi ya soka daraja la tatu Wilaya ya Kaskazini ‘A’ kati ya
timu hiyo na Amber Sports Club zote za Matemwe, katika mchezo huo
uliochezwa uwanja wa New Stars Mkwajuni
WACHEZAJI
wa Timu ya Amber Sports Club inafadhiliwa na Kampuni ya Pennyroyal wakisaliana
na timu ya Kijini zote za Matemwe wakati wa pambano lao la soka ligi daraja la
tatu wilaya ya Kaskazini ‘A’,
MCHEZAJI wa
Timu ya Amber Sports Club , Mwadini Ame akitafuta mbinu za kumtoka mlinzi wa
timu ya Kijini Stars, Bakar Kassim, zote za matemwe wakati wa pambano lao la
ligi ya soka wilaya ya Kaskazini ‘A’, katika mchezo huo uliochezwa uwanja wa
New Stars Mkwajuni, amber ilishinda mabao 6-0.
MSHAMBULIAJI
wa Timu ya Amber , Hussein Issa Muumin akipiga ngema baada ya kushinda bao la
kwanza katika mchezo wa soka ligi daraja la tatu wilaya ya Kaskazini ‘A’ kati ya timu hiyo na Kijini Stars zote za Matemwe,
katika mchezo huo uliochezwa uwanja wa New Stars Mkwajuni, amber inayofadhiliwa
na Kampuni ya Pennyroyal ilishinda mabao 6-0 .
Baadhi wa Mchezo wa mpira katika Kijiji cha Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakifuatilia mchezo Ligi Daraja la Pili uliozikutanisha Timu za Amber na Kijini Stars zote kutoka katika kijiji cha matemwe.
No comments:
Post a Comment