Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Ashiriki Katika Hafla ya Chakula cha Mchana na Vijana na Wanafunzi Walioshiriki Halaiki Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar Amaan.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Katibu wa Halaiki Zanzibar Ali Mohammed Bakari, alipowasili katika viwanja vya Kikosi cha KVZ Mtoni kuhudhuria hafla hiyo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar baada ya kumaliza hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili ya Vijana hao katika Viwanja vya KVZ Mtoni
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, wakijumuika na Vijana na Wanafunzi walioshiriki katika Halaiki ya kuadhimisha Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

BAADHI ya Wanafunzi na Vijana walioshiriki sherehe za maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar wakishiriki katika hafla ya chakula maalum cha mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, katika kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar
VIJANA wa Bendi ya Chipukizi wakitoa burudani wakati wahafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili ya Vijana na Wanafunzi walioshiriki katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar

BAADHI ya Wanafunzi na Vijana walioshiriki katika sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar, wakijumuika katika hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,kilichofanyika katika viwanja vya Vikosi vya KVZ Mtoni Zanzibar

WAZIRI wa Nchi na Afisi ya Rais Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu akitowa neno la shukrani wakatika kumalizika kwa Hafla ya Chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzinar kwa ajili yao kilichofanyika katika Kambi ya Vikosi vya KVZ Mtoni Zanzibar.





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.