Habari za Punde

Mahafali ya Chuo cha Amali Mkokotoni


Wanafunzi wa Chuo cha Amali Mkokotoni wakionyesha mchezo wa maigizo kuonyesha athari zinazowakuta wanafunzi wanapojuhusisha na matumizi ya dawa za kulevya wakati wa masomo katika mahafali ya tano ya Kituo cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja . Picha na Miza Othman-Maelezo Zanzibar.
 Wanafunzi wakionyesha matokeo ya masomo  yanayowapata wanafunzi kutokana na kutokana na matumizi ya Dawa za kulevya. Picha na Miza Othman-Maelezo Zanzibar.
 Mbunge wa Jimbo la Tumbatu Juma Othman Hija akiwapa nasaha wanafunzi waliyohitimu  Mafunzo ya Ufundi katika Chuo cha Amali Mkokotoni  akiwa Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo. Picha na Miza Othman-Maelezo Zanzibar.
 Mgeni Rasmi  akimkabidhi Cheti mmoja wa wahitimu Vuai Silima Juma  katika Mahafali yaliyofanyika Chuoni hapo. Picha na Miza Othman-Maelezo Zanzibar.
 Mmoja wa Wanafunzi Pili Omar Jafar  katika fani ya Ushoni akizawadiwa zawadi ya Henga ya Nguo na walimu wake baada ya kufanya vizuri katika masomo yake. Picha na Miza Othman-Maelezo Zanzibar.
 Mgeni Rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Walimu wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja. Picha na Miza Othman-Maelezo Zanzibar.
Mgeni Rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa  fani mbalimbali wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja. Picha na Miza Othman-Maelezo Zanzibar.


Na Ali Issa Maelezo 
Vijana wanaomaliza mafunzo katka Vituo na Vyuo vya mafunzo ya Amali Zanzibar wametakiwa kutumia fursa ya mafunzo wanayoyapata kujiajiri wenyewe ili na kusubiri ajira Serikalini.
Hayo yamesemwa leo huko Kituo  cha Mafunz oya Amali Mkokotoni Mkoa wa kaskazini Unguja na Mbunge w ajimbo la Tumbatu Juma Othuman Haji wakati wa utoaji wa vyeti katika mahafali ya tano ya kituo hicho kwa wanafunzi wa kozi mbambali waliomaliza mafunzo yao .
Amesema si vyema kwa wanafunzi hao kumaliza masomo yao na kupata vyeti vya kitaalamu baadae vijana hao kushindwa kujiajiri wenyewe na badala yake kujiingiza katika makundi yaliokata tamaa na kujiunga katika dimbwi la maovu.
Itumieni fursa hii kujiajiri kwani sasa serikali imeweka vituo hivi ili vijana wake waweze kujiajiri wenyewe nasi vyema vyeti hivi vikaishia hapa na ujuzi kupotea”,alisema Mbunge huyo.
Aidha alisema kuwa kuna baadhi ya vijana wana tabia ya kuipuuza elimu yaamali lakini watambue kwamba duniani kote elimu ya amali hutumika kuwakombowa vijana na kuwa waledi kujitafutia riziki zao.
Alifahamisha kuwa vyuo vya Amali vimekuwa vikitoa watalamu mbalimbali ambapo wengi wao wameshika nyadhifa serikalini na klitumikia taifa.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Bakari Ali Silima Kituo hicho kimekuwa kikitoa kozi mbalimbali ikiwemo ufundi ushoni, ufumaji, umeme,umeme wa magari na elekroniki, fundi mafriji na viyoyozi, fundi muwashi, seremala, upishi, upambaji,miferiji, udereva na ukodishaji wa mashamiani utaanza mwakahuu.
Hata hivyo aliwataka wahitimu hao kukaa kwa vikundi ili kuweza kuanzisha miradi kwa kupatiwa zana za kufanyia kazi kwa lengo la kujendeleza kimaisha
alisema kuwa chuo hicho hivi karibuni wametia komputa 50 na vifaa vyengine vya kutosha ambavyo vitatumika kwa kusomeshea kwa viendo ili kuwapa uelewa zaidi wanafunzi wao.
Mapema wakisoma risala walisema kuwa Kituo hicho kimekuwa kikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa maji na uzio pamoja na nyumba za walimu na dakhalia kwa wanafunzi jambo ambalo linaleta usumbufumkubwa kituoni hapo. 

3 comments:

  1. ningependa kufanya kazi nanyi.. chuo cha ufundi

    ReplyDelete
  2. Sorry naomba email ya chuo hiki
    ntumie kwenye e-mail yangu

    ReplyDelete
  3. Jee wanasomesha ufundi taizi

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.