Habari za Punde

Mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba afanya ziara ya kushtukiza Skuli ya Sekondari ya Moh'd Juma Pindua, Mkoani Pemba

 Skuli ya Sekondari ya Moh'd  Juma Pindua ambapo mkuu wa Mkoa wa Kusini pemba alifanya ziara ya kushtukiza


 Mh Hemed Suleiman Abdalla akizungumza baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Skuli ya Sekondari ya Moh'd  Juma Pindua

Na Salmin Juma, Pemba
Mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba Mh Hemed Suleiman Abdalla leo amefanya ziara pasi na taarifa katika skuli ya sekondari ya  Moh'd  Juma Pindua  huko Michenzani wilaya ya mkoani kwa lengo la kujionea hali halisi ya mazingira kwa wanfunzi yanavyokua katika maeneo yao pomoja na shida za walimu.

Mkuu wa mkoa aliambatana na katibu wake pamoja na viongozi wengine katika zira hiyo.

Akizungumza mara baada ya zira hiyo Mh Mkuu wa mkoa amesema ameridhishwa na hali jinsi ilivyo katika skuli hiyo maana kama kungekuwepo na mapungufu makubwa angeliyaona kwasababu ziara yake ilikua ni ya kushtukiza.

Amesema changamoto walizozigundua ni za kawaida na wapo mbioni kuhakikisha  zinaondoka na wanafunzi wanakua katika mazingira mazuri ya kujisomea

"Wanafunzi wameniambia ,  hawana mwalimu wa somo la civics  pamoja na huduma ya maji, haya tunayajua na tupo mbioni kuyatatua lakini kwa ujumla hali inakwenda vizuri" amesema mkuu wa mkoa

Wanafunzi wa skuli hiyo wamefurahika sana kutokana na ziara hiyo  na walikua huru kueleza hisia zao kutokana na fursa waliyopewe.

Mmoja miongoni mwa wanafunzi wa skuli hiyo Sumaiyya Abdalla wa kidato cha pili amesema anawaomba viongozi kujitahidi kupigia mbio changamoto zao ikiwamo hiyo wa maji ili waendele kubaki salama.

Nae Kauthar Ali amesisitiza kupatikana mwalimu wa somo hilo la la civics jambo ambalo Mh Hemed ameahidi kulitatua haraka  iwezekanavyo.

Katika ziara hiyo Mh Hemed amewataka wanafunzi kuachana na mambo yasiowahusu na badala yake wajikite zaidi katika masomo ili wapate matokeo mazuri huku akiahidi kuwa hali ya ufaulu mara hii itabadilika kutokana na juhudi wanazozichukua.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.