Habari za Punde

Mazishi ya Pacha Maria na Consolata Yaliofanyika leo Tanzania Mkoani Iringa.







Wananchi wa Iringa wakiwa na simanzi wakati wa mazishi ya Watoto walioungana Maria na Consolata yaliofanyika leo. 
Walipofaulu mtihani wa kidato cha sita, walieleza furaha yao kuu baada ya kufaulu mtihani na kueleza ndoto zao.
"Tulipokea matokeo yetu tukiwa kwenye mazingira ya nyumbani tu, tukiendelea na shughuli zetu za kila siku, tukaambiwa matokeo yametoka na tumefanya vizuri, tulikuwa tukiwaza kabla ya hapo, unajua kwenye mitihani ya mwisho huwezi kujiamini sana," alieleza Consolata.


Watu wengi wamejitokeza asubuhi ya leo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) eneo la Iringa katika ibada maalumu ya kuwaaga pacha waliokuwa wameungana Maria na Consolata waliofariki mwishoni mwa juma.
Miongoni mwa waliofika ni viongozi mbali mbali wa dini na kiserikali.Baada ya ibada kutakuwa na maandamano ya kuelekea katika makaburi ya Tosamaganga ambapo ndipo miili yao itakapopumzishwa.
Askofu Jimbo Katoliki Njombe, Alfred Maluma amesema vifo vya Pacha hao vinafaa kutumiwa na Watanzania kukumbushana wajibu wao kwa watu wenye ulemavu.
"Wameacha somo hilo, tuwajali watu wenye ulemavu hilo ndilo somo walilotuachia Maria na Cobsolata."
Amesema Mungu aliwaumba pacha hao kwa mfano wa sura yake na akawapa uhai kwa kipindi walichokuwa duniani. Vifo vya Maria na Consolata ambao walikuwa ni wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Ruaha vimegusa wengi hasa kutokana na ujasiri walioonyesha wakati wa uhai wao.
Vile vile watakumbukwa kwa ucheshi wao.
Pacha hao wameandaliwa jeneza moja lenye mfumo wa watu wawili, misalaba miwili na watazikwa katika kaburi moja.
Mkuu wa Shirika la Maria Consolata, Jane Nugi alikuwa ameambia gazeti la Mwananchi kwamba pacha hao waliamua eneo ambalo watazikwa.
Alisema katika uhai wao walichagua kuzikwa kwenye eneo wanalozikwa viongozi wa kanisa Katoliki eneo hilo.


"Wakati wakiumwa walisema wangetamani kuhifadhiwa tunakohifadhiwa sisi hivyo watazikwa kwenye makaburi ya Tosamaganga," alisema.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.