Habari za Punde

Benki ya Credit Suisse Kuipatia Tanzania Mkopo Nafuu wa Shs. Bilioni 450 Kujenga Reli ya Kisasa na Umeme.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango akipokea picha ya alama ya ushirikiano ya kiasi cha Dola 500 kutoka kwa Afisa mwandamizi wa Benki ya Suisse ya Uingereza Bi. Elizabeth Muchemi, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia) akiwa kwenye majadiliano na ujumbe kutuko Benki ya Credit Suisse, ambapo Benki hiyo inasaidia maswala mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo kusaidia kwenye Sekta na Maji, Barabaraba na Umeme, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. 
Mchumi Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Omary Khama (kulia), anayeshughulika na maswala ya uchambuzi wa madeni akimwelezea Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia) kuhusu miradi mbalimbali itakayotekelezwa kutokana na pesa iliyopatikana, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Benki ya CREDIT SUISSE. 

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (kulia) akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wea Benki ya Suisse Bw. Lawrence B. Fletcher kwa mikopo mbalimbali ambayo Benki hiyo imetoa kwa Serikali ya Tanzania katika Sekta mbalimbali, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.