Habari za Punde

Timu ya Walimu 14 wa Masomo ya Hesabati na Fizikia Kutoka Nchini Nigeria Wawasili Zanzibar Tayari Kutowa Elimu ya Masomo Hayo Kwa Wanafunzi wa Sekondari wa Unguja na Pemba.

Afisa Elimu Sekondari Mwali Khalifa Rashid akisalimiana na Mkuu wa Msafara huo Mkurugenzi Mipando Dr.Lawal Bappah baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege ya Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar na Timu ya Walimu wa Masomo ya Hesabati na Fizikia,Ikiwa na awamu ya Pili ya Walimu hayo kuwaili Zanzibar awamu ya kwanza ikiwa na Walimu 23 na kufanya Jumla ya Walimu wa Masomo ya Hesabati na Fizikia kutoka Nchini Nigeria kufikia 37. Watawafundisha Wanafunzi wa Skuli za Sekondari Zanzibar.
 Afisa wa Ubalozi wa Nigeria NchiniTanzania akisalimiana na Afisa Elimu ya Sekondari Zanzibar baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
Afisa Elimu Sekondari Zanzibar Mwalimu Khalifa Rashid akiongozana na Mkuu wa Msafara wa Walimu wa Masomo ya Hesabati na Fizikia kutoka Nchini Nigeria Mkurugenzi Mipango Dkt. Lawal Bappah, wakitoka katika majengo ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, baada ya kukamilisha taratibu za uhamiaji kiwanjani hapo.

Walimu wa Masomo ya Hesabati na Fizikia kutoka Nchini Nigeria wakiwasili Zanzibar kwa ajili ya kuja kufundisha Masomo hayo kwa Wanafunzi wa Skuli za Sekondari za Unguja na Pemba. 



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.