Habari za Punde

Bi. Zuwena Salum Said Amepewa Nafasi ya Kukaa Jumba la Treni Kwa Muda Wake Wote wa Maisha Yake Bila ya Kulipa Kodi.

Muonekano wa Jengo la Jumba la Treni Darajani baada ya kumalizika ukarabati wake Mkubwa uliofanywa na Kampuni ya Kichina ya CRJE ,Jengo hilo ni moja ya miradi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF.).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Bi. Zuwena Salum Said, baada ya kumalizika kwa hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi na Uzinduzi wa Jengo la Jumba la Treni, baada ya kumalizika ujenzi wake mkubwa wa maduka ya kisasa na Sehemu ya Mazoezi ya Gym, Nyumba za Makaazi, Mgahawa na Maduka.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud amesema Bi. Zuwena amepewa Ofa ya kukaa katika moja ya nyumba za jengo hilo la treni kwa muda wake wote wa maisha bila ya bughudha yoyote, baada ya kukamilika taratibu za kisheria. 

Bi Zuwena ni mmoja wa Mwananchi aliyekuwa akiishi katika nyumba hiyo na kuchukua muda kuhama baada ya wapangaji wate kuha ili kupisha ujenzi wake mkubwa uliofanywa na Kampuni ya Kichina ya CRJE. 

Busara za Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud kuzungumza nae na na kukubai kuhama na kuhamia katika nyumba za wazee sebleni amekaa kwa muda na kuchukuliwa na Jamaa zake na kuhamia katika mtaa wa mkunazini Unguja anakoishi mpaka sasa katika eneo hilo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Bi. Zuwena Salun Said, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja na kulia Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Abdllah Mwinyi Khamis, walipiga picha hiyo baada ya kumalizika kwa hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi na Uzinduzi wa Jengo hilo baada ya kumalizika kwake kwa ujenzi wake mkubwa uliofanywa na Kampuni ya Kichina ya CRJE.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.