Habari za Punde

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Azungumza na Wafanyakati wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar Akiwa Katika Ziara Yake Kutembelea Idara za Wizara Yake.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria na Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman akisalimiana na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Mzee.Ali Haji, alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar katika eneo la Mazizini Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman akisalimiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Said Hassan Said, baada ya kuwasili katika Ofisi za Mwanasheria Mkuu Mazizini Zanzibar, wakati wa ziara yake kutembelea Ofisi zilizo katika Wizara yake.  
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman akiongozana na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Mzee.Ali Haji, wakielekea ukumbi wa mkutano kuzungumza na Wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa ziara yake.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Said Hassan Said akizungumza na kutoa taarifa ya Utendaji kazi wa Ofisi yake wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman, wakati wa ziara yake alipotembelea Ofisi hiyo. 
Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ndg. Yakout akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman, kuzungumza na Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mazizini Zanzibar wakati wa ziara yake kutembelea katika Ofisi zilizo katika Wizara yake.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman akizungumza na Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa ziara yake kutembelea  Ofisi hiyo kupata changamoto wanazokabiliana nazo wakati wa Utendaji wa kazi zao za kushimimia Sheria Zanzibar.
Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar wakifuatilia Mkutano huo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman alipofanya ziara kutembelea Ofisi hiyo ilioko katika Wizara yake.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utawala wa Umma na Utumishi Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman alipokuwa akizungumza na Uongozi na Wafanyakazi wa Ofisi hiyo. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.