Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akikagua moja ya makazi ya askari
polisi katika kijiji cha Makongoro B, kilichopo wilayani Bunda wakati wa ziara ya
kikazi ya kukagua na kushughulikia changamoto za makazi ya askari polisi ambapo jumla ya nyumba mia nne za askari polisi zinatarajiwa kujengwa nchi
nzima
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisoma maelezo ya mmoja ya mtuhumiwa aliyemkuta katika chumba cha mahabusu katika
Kituo cha Polisi Bunda wakati wa ziara ya kikazi ya kupitia shughuli za
utekelezaji wa mashtaka ya mahabusu walioko katika vituo vya polisi nchini.Wapili
kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili na wengine ni viongozi
waandamizi wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Bunda
Afisa Mnadhimu wa Polisi mkoa wa Mara, Mrakibu Mwandamizi
,Jeremiah Shila akitoa maelezo ya mwenendo wa mashtaka ya
watuhumiwa walioko katika Kituo cha Polisi Bunda kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili
kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia
Bupilipili(watatu kulia), wakati wa ziara ya naibu waziri kupitia shughuli za utekelezaji wa mashtaka
ya mahabusu walioko katika vituo vya polisi nchini.
Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani
ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu
kushoto), akifuatilia wakati mpelelezi akifunua jalada la mmoja wa mahabusu
aliyemkuta katika chumba cha mahabusu katika Kituo cha Polisi Bunda
wakati wa ziara ya kikazi ya kupitia shughuli za utekelezaji wa mashtaka ya
mahabusu walioko katika vituo vya polisi nchini.Wapili kulia ni Mkuu wa Wilaya
ya Bunda, Lydia Bupilipili na wengine ni viongozi waandamizi wa kamati ya
Ulinzi na Usalama wilayani Bunda.Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
No comments:
Post a Comment