Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Ziarani Nchini Oman.

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud Kushoto akimtakia safari njema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyeondoka Zanzibar kupitia Dar es salaam akielekea Nchini Oman kwa ziara Maalum. 
Mfanyakazi wa Kampuni ya Ndege ya As salam Luck akimkaribisha Balozi Seif kwenye ndege yao iliyomchukua hadi Mjini Dar es salaam akielekea Nchini Oman kwa ziara Maalum. Picha na – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameondoka Zanzibar leo mchana kupitia Jijijini Dar es salaam kuelekea Nchini Oman kwa ziara Maalum.
Balozi Seif  Ali Iddi katika safari hiyo Maalum anafuatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi pamoja na baadhi ya Wasaidizi wake  wa kazi.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliagwa na Viongozi mbali mbali wa Serikali, Vyama vya Siasa pamoja na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Serikali zote mbili Nchini Tanzania.
Balozi Seif  na Ujumbe aliofuatana nao anatarajiwa kurejea Nyumbani  Zanzibar Tarehe 04 Novemba Mwaka 2018.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.