Habari za Punde

Wajumbe wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Watembelea Ujenzi wa Majengo Pacha Yanayojengwa Katika Eneo la Gombani Kisiwani Pemba.

Muonekano wa Majengo Pacha yanayojengwa katika eneo la Gombani Kisiwani Pemba , yatakapomalizika Ujenzi wake yatatumika na Wizara Tatu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , kwa ajili ya Ofisi zake, Wizara hizo ni Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria na  Utawala Bora, Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto na Wizara ya Fedha na Mipango.  
Tranfoma za Umeme zitakazotumika katika majengo hayo zikiwa tayari zimefungwa na kutowa huduma ya Umeme baada ya kukamilika ujenzi huo na kuweza kutoka huduma hiyo katika majengo hayo Pacha katika eneo la Gombani Kisiwani Pemba.
 AFISA Mdhamini Wizara ya Fedha na Mipango Pemba Ibrahim Saleh Juma, akitoa taarifa ya Kitaalamu juu ya ujenzi wa majengo pacha ya Wizara tatau za Serikali huko Gombani, kwa wajumbe wa kamati ya Fedha Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi zanzibar wakati wa lipotembelea jengo hilo
WAJUMBE wa Kamati ya Fedha Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakipata maelezo ya kifaa cha kisasa cha kutolea ishara ya hatari ya moto, kutoka kwa fundi mkuu wa Kampuni ya QBC Ali Abdalla, wakati walipotembelea majengo pacho yanayoendelea kujengwa huko Gombani.
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA) 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.