Habari za Punde

Balozi Seif Afungua Hospitali ya Meno.




Na.Othman Khamis OMPR.
Mlezi wa Mkoa wa Shinyanga Kichama ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewakumbusha Wananchi kuwatafuta Viongozi walioshiba Maadili wakati wa chaguzi tofauti zinapokaribia kwa vileViongozi hao hujali Uzalendo wao katika moyo wa  kuwatumikia kimaendeleo.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa angalizo hilo wakati akizungumza na Wanachama wa CCM pamoja na Wananchi wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga mara baada ya kukabidhi Kiti cha huduma za Meno Mwenye Hospitali ya Wilaya ya Jakata Kikwete alichowaahidi Wananchi hao wakati wa ziara yake ya kujitambulisha Miezi Miwili iliyopita.
Kiti hicho pia kilijumuisha pia na Kiti cha kuchukulia Wagonjwa Magongo kwa Wagonjwa wenye Ulemavu wanaohitaji kuingia kwa Daktari pamoja na Vifaa vidogo vidogo vya kuwasaidia Madaktari kujikinga na maambukizo ya maradhi mbali mbali.
Alisema wakati wa kufikiria kuwa na mlolongo wa Viongozi wenye upofu wa kutoona maendeleo makubwa yaliyofanywa na Chama cha Mapinduzi katika Utekelezaji wa sera na Ilani yake, wapenda madaraka pamoja na  walafi kwa sasa umemalizika kabisa.
Balozi Seif alisema Wananchi wa Wilaya ya Kishapu wamebarikiwa kuwa na Viongozi makini katika kutanzua Kero zinazowakabili. Hivyo wana kila sababu ya kuwaunga mkono katika kutimiza kiu yao ya kuwaletea maendeleo sambamba na Kutekeleza Inali ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020.
Mlezi huyo wa Mkoa wa Shinyanga aliwahakikishia Wananchi hao kuendelea kuwaunga mkono kwa kuchangia huduma za Afya ambazo ni za msingi katika Ustawi wa maisha na Afya zao za kila siku.
Aliwataka kujenga Utamaduni wa kupima Afya zao badala ya ile tabia ya kusubiri maradhi yanapojichomoza kwa Vile Serikali Kuu kupitia Halmashauri za Wilaya mbali mbali Nchini tayari zinaendelea kujenga miundombinu imara katika Sekta ya Afya.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Kishapu pamoja na Mkoa mzima wa Shinyanga Mkuu wa Mkoa huo Mh. Zainab Telak alisema kitendo alichofanya Mlezi  huyo ni Moja ya Ibada ya kuwasaidia Wananchi wataoitumia Hospitali hiyo katika kupata huduma za Afya.
Mh. Zainab alisema msaada wa Mlezi huyo wa Mkoa wao  anayejali Afya za Watoto wake umeenda sambamba na jitihada za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarisha Miundombinu ya Hospitali za Wilaya Nchini.
Alisema kuanzia sasa huduma za matibabu ya maradhi ya Meno zitatolewa na Wataalamu Wawili  Wazalendo waliopo katika Hospitali hiyo ya Jakaya Kikwete badala ya mfumo wa zamani wa wagonjwa kufuata huduma hiyo katika masafa marefu ya iliyopo Hospitali ya Mkoa.
Mapema asubuhi Balozi Seif alianza ziara yake ya Ulezi  kwa kukuagua Uzalishaji wa Mchele katika Kiwanda cha Kusaga Mpunga { Miran Food Industries} kiliopo Lohumbo Mkoani Shinyanga.
Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho Bwana Tano Koleji alimueleza Mlezi huyo kwamba Kiwanda hicho kimejengwa Mnamo Mwaka 2017 na kuanza uzalishaji rasmi Mwaka uliofuatia wa 2018 kikiwa na wafanyakazi wa 80 wa kibarua na Wanne waliopata ajira za kudumu.
Bwana Tano alisema wapo Wakulima wanaoamua kuhifadhi Mpunga wao kwenye ghala la Kiwanda hicho kwa lengo la kutafuta wateja na pale wanapopatikana husagiwa mpunga kwa kiwango wanachohitaji katika ununuzi wao.
Hata hivyo Meneja huo wa Miran Food Industries alieleza kwamba zipo changamoto zinazokikabili Kiwanda hicho ikiwa ni ukosefu wa Wateja wa Ununuzi wa Mchele wakati uzalishaji kwa siku unafikia Tani 30 lakini wanunuzi hawazidi Nusu Tani tu.
Akitoa nasaha zake Balozi Seif  aliutaka Uongozi wa Kiwanda hicho kutokata tamaa kwa vile bidhaa za Mchele bado inahitajika katika masoko mbali mbali ndani na nje ya nchi lakini kinachokosekana ni mawasiliano tu.
Kiwanda cha Milan kina uwezo wa kuzalishaji mchele wa daraja la kwanza  wanaouuza kwa kima cha shilingi Elfu 1,800/- kwa ujazo wa  Kilo moja.
Akishiriki kazi za ujenzi wa Taifa baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Shinyanga Vijijini Mlezi wa Mkoa wa Shinyanga Balozi Seif alisema kazi inayofanywa na Wana CCM wa Shinyanga ya uimarishaji wa Chama inafaa kuigwa na Mikoa mengine Nchini.
Balozi Seif  alisema miradi ya Chama inayotekelezwa ndani ya Kata, Majimbo na Wilaya zilizomo ndani ya Mkoa wa Shinyanga na kusimamiwa vyema na Viongozi wao zimekuwa zikisaidia kuipeperusha Benderra ya CCM katika muelekeo wa Utekelezaji sahihi wa malengo yake.
Alisema viongozi bora ni wale wanaosimamia mambo yanayowagusa moja kwa moja Wananchi kama inavyoonekana Mkoani Shinyanga na Wilaya pamoja na Kata zake.
Balozi Seif alifahamisha kwamba miradi ya huduma za Maji, Afya, Bara bara pamoja na Elimu endapo inasimamiwa na kutekjelezwa vilivyo hakuna haja kwa Wananchi kubadilisha Viongozi wengine katika kuwasimamia kwenye neema hizo.
Hata hivyo Balozi Seif alisisitiza umuhimu wa Wanafunzi kuonyesha juhudi katika Sekta ya Elimu inayowanjengea mazingira mema ya muelekeo wa maiksha yao ya baadae wakiwa wao ndio watakaokuwa wasimamizi wa kuliendesha Taifa la Tanzania.
Akisoma risala ya Ujenzi wa Ofisi hiyo ya CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya hiyo Nd. Jumanne Kilindu alisema wazo la kuanzishwa kwa jengo hilo inatokana na ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dr. Bashir Ali aliyeuagiza Uongozi wa Wilaya hiyo kujenga Ofisi ya kudumu.
Nd. Jumanne alisema Wana CCM wa Wilaya ya Shinyanga Vijijini iliyozaa Shinyanga Mjini na Kishapu  walianmza harakati za ujenzi chini ya Timu ya Madiwani wa Wadi zilizomo ndani ya Wkilaya hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wao wa Halmashauri.
Kabla ya hapo Balozi Seif alikagua maendeleo ya Ujenzi waMajengo Mapya ya Hospitali ya Wilaya ya Shinyanmga Vijijini, ujenzi unaokwenda sambamba na ule wa Hospitali ya Kishapu zilizotengewa na Serikali Shilingi Bilioni Tatu.
Balozi Seif aliafikiana na uamuzi wa Serikali ya Mkoa huo kuwatumia Wahandisi Wazal;endo katika Ujenzi huo badala ya kutumia Wakandarasi wenye tabia ya kuhitaji gharama kubwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.