Habari za Punde

Mashua yakamatwa Pemba ikiwa na bidhaa za magendo na Mirungi

Na Masanja Mabula-PEMBA
KIKOSI  maalumu ya kuzuia magendo KMKM Kamandi ya Pemba kimefanikiwa kukamata mashuwa ambayo ilikuwa imesheheni bidhaa mbali mbali za magendo  ikiwemo dawa za kulevya aina ya mirungi ikitokea Mombasa Kenya kuja kisiwani Pemba.
Mkuu wa Operesheni kikosi cha KMKM Kamandi ya Pemba luteni Mchumi Koja Mchumi akizungumza Ofisini kwake amesema mashuwa hiyo ilikamatwa na askari wa kikosi hicho waliokwua katika doria za kawaida.
Kamanda Mchumi amesema baada ya kufanya upekuzi wakabaini uwepo wa mafurushi hamsini na moja ya mirungi.
Aidha mwanasheria wa KMKM Kamandi ya Pemba Omar Maulid Juma amesema jukumu la kikosi hicho ni kukamata na kuzikabidhi mamlaka husika.
Amefahamisha kwamba mamlaka ambayo wanashirikiana ni ZAECA  na kuongeza kwamba tayari watumhumiwa hao wamewakanbidhi kwa ZAECA.
Afisa Dhamana wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi ZAECA Pemba sulemain juma ame amesema kwa mujibu wa sheria ya ZAECA watuhumiwa hao wanayo kesi ya kujibu.
Watu waliokuwemo ndani ya mashuwa hiyo ni Nahodha Abdalla Kombo , mabaharia Makame Faki na Ali Makame ambapo abiria waliokuwamo ni Omar Mohd Juma aliyekamatwa na mafurushi tisa ya mirungi(9)pamoja na Anwari Maalim Said  yeye amepatikana na mafurushi 42

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.