Habari za Punde

Wane wafariki dunia katika ajali ya gari

Watu wanne wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyoacha njia na kupinduka eneo la Kibuteni na mwengine kupelekwa hospitali ya Mnazi Mmoja kwa ajili ya matibabu Wilaya ya Kusini Unguja Mkoa wa Kusini Unguja.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Suleiman Hassan Suleiman amesema ajali hiyo imetokea siku ya terehe 22 ya mwezi huu majira ya saa nane na robo Usiku huko Kibuteni.

Ameongeza kusema kuwa waliofariki katika ajali hiyo wametambulika kwa majina ya Lutifia Abdalla Abdalla anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20-25 Mkaazi wa Muembe Ladu, Dereva wa gari Bakari Muharami Bakari mwenye umri wa miaka 24 mkaazi wa Ubago, Suleiman Kassim Ameir mwenye umri wa miaka 18 , Rafii Hassan Haji mwenye Umri wa miaka 24 mkaazi wa Ubago pamoja na Majeruhi Jabir  Kassim Ameir mwenye Umri wa miaka 21 Mkaazi wa Ubago .

Sambamba na hayo Kamanda Suleiman ametoa wito kwa madereva wa vyombo vya moto kuwa na tahadhari katika utumiaji wa barabara na kuwataka kupunguza mwendo kasi wa gari zao ili kuweza Kuepuka  ajali zisizo za lazima

Ajali hiyo iliyohusisha gari aina Toyota Mark II  yenye namba za usajili Z310 HM iliyokua ikitokea makunduchi kuelekea mjini ilipofika Kibuteni iliacha njia na kupinduka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.