Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye(wa pili kutoka kushoto) akiambatana na Msemaji Mkuu wa Serikali,Dkt.Hassan Abbasi (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi mtendaji wa TAZARA-Zambia, Mhandisi.Bruno Chingandu (wa kwanza kulia) na Meneja wa TAZARA ,Mkoa wa Tanzania, Fuadi Abdallah wa pili kulia wakiwa katika uzinduzi wa mitambo ya kunyanyulia mizigo stesheni ya Fuga.
Na.Paschal Dotto-Maelezo Dar es Salaam. 20-08-2019.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Mhe.Atashasta Nditiye amazindua Rasmi Vifaa vya Kunyanyulia Makontena ya Mizigo
na Vifaa vizito vya utekelezaji wa ujenzi wa Mradi mkubwa wa umeme wa Julius
Nyerere Hydro Power Project (JN HPP).
Akizungumza jana katika stesheni ya fuga, Waziri
Nditiye alisema kuwa Serikali imenunua vifaa hivyo ambavyo ni Reach Stacker 2 zenye uwezo wa kunyanyua
tani 45, Mobile crane yenye uwezo wa
tani 15 na Forklift 2 zenye uwezo wa
tani 5 na zimegharimu Tzs Bilioni 3.5
“Vifaa hivi vimenunuliwa na Serikali ili kuiwezesha
TAZARA kutekeleza majukumu iliyopewa ya upokeaji makontena ya mizigo mizito ya
ujenzi wa bwawa la kufua umeme la JN HPP, katika mto Rufiji, mradi utakozalisha
Megawati 2,115 na kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa viwanda”, Naibu Waziri
Nditiye.
Aidha, Waziri Nditiye alisema kuwa Serikali itaendelea
kuishika mkono TAZARA ili kuhakikisha inafanya kazi ufanisi mkubwa kwenye
utekelezaji wa mradi wa kufua umeme JN
HPP na ndiyo maana imetoa Tsh. Bilioni 10 ili kununua Traction Motors 42 kwa ajili ya vichwa saba vya treni za masafa
marefu na sogeza ambazo zitaanza kuwasili mwezi oktaoba.
Waziri Nditiye aliongeza kuwa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inawahakikishia wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli Tanzania na
Zambia (TAZARA)kuwa itaendelea kulipa mishahara yote kwa kipindi chote cha
mwaka wa fedha 2019/2020 na tayari imetanga kiasi cha shilingi bilioni 14.9
zimetengwa.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Mamlaka ya Reli ya
Tanzania na Zambia (TAZARA) alisema kuwa ni
jambo kubwa na heshima kwa Mamlaka hiyo kupewa majukumu ya kupoea mizigo
ya utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa Umeme JN HPP.
“Napenda kusema kuwa Serikali ya Tanzania, Chini ya
Rais Dkt.John Pombe Magufuli, ilituamini na kutupatia kiasi cha Shilingi
Bilioni tano ili kukarabati stesheni ya Fuga kwa kujenga Stendi ya kupokea na
kusafirisha mizigo, kununua vifaa vitakavyosaidia kunyanyua mizigo hiyo kwa
ufanisi mkubwa”, Mhandisi. Bruno Chingandu.
Mhandisi Chingandu alisema kuwa vifaa hivyo viyakuwa
na uwezo mkubwa wa kutosheleza mahitaji ya kupokea mizigo ya ujenzi wa mradi
mkubwa wa kihistoria wa kufua umeme wa
JN HPP, kwani tani kati ya 5 mpaka 45 zitanayanyuliwa na vifaa hivyo.
Aidha, Mhandisi Chingandu alisema kuwa Serikali
imetekeleza kwa vitendo ununuzi wa Traction motor 42 kwa ajili ya treni ya
masafa marefu kwa kutoa Tsh.Bilioni 10, hivyo itaiwezesha TAZARA kutekeleza majukumu
yake kwa ufanisi mkubwa na kuliwezesha Shirika hili kurejera tena katika
utendaji mkubwa.
Naye Meneja wa TAZARA Mkoa wa Tanzania, Fuad Abbdalah,
alisema kwamba Serikali imewapatia Fedha za ujenzi na ununuzi wa vifaa ni
heshima kubwa kwa Shirika hilo kwani limeingia kwenye historia ya mageuzi ya
Serikali ya Awamu ya Tano.
“Leo tunashuhudia kitendo kikubwa cha kuzindua hizi
mashine tano za kunyanyulia mizigo mizito ya ujenzi wa Mradi wa kihistoria wa
JN HPP, Mashine hizi zina uwezo mkubwa wa kunyanyua Tani 5 mpaka 45, uwezo
stahiki kabisa kuhudumia mizigo yote inayohitajika kwenye mradi wa umeme mto
Rufiji”; Fuad Abbdalah, Meneja TAZARA mkoa wa Tanzania
Fuad aliongeza kuwa Serikali imeliamini Shirika hilo
na Rais wa Jamhuri ya Muungano ameahidi kurudisha uafanisi wa utendaji wake na
katika ziara yake ya kwenda kuzindua Mradi wa umeme JN HPP alisema atahakikisha anashirikiana na Rais wa Zambia
ili kurudisha heshima ya TAZARA.
Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan
Abbasi alisema Serikali imetekeza ukarabati wa stesheni ya kupokea na kushushia
mizigo ya Fuga itayosaidia ujenzi wa Mradi wa Umeme wa JN HPP kufanikiwa kwa
haraka Zaidi.
“Tunatekeleza Uboreshaji huu wa Stesheni ya Fuga,
tumeleta mitambo ya kisasa mikubwa kabisa ambayo imedhaminiwa na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kuhudumia ujenzi wa bwawa la kufua
umeme JN HPP, kwa hiyo mitambo hii imefika, inafanya kazi na inasambazwa na
Kampuni ya kizawa”, Dkt.Abbasi.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye(wa pili kutoka kushoto) akivaa kofia kujiandaa kuwasha moja ya mitambo ya kunyanyulia mizigo ya ujenzi wa mradi wa Umeme JN HPP iliyopo katika Stesheni ya Fuga, wa kwanza kushoto ni Meneja wa TAZARA ,Mkoa wa Tanzania, Fuadi Abdallah.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye, akiendesha moja ya mitambo ya Kunyanyulia mizigo iliyoko katika stesheni ya Fuga wakati wa ufunguzi wa mitambo hiyo hapo jana Agosti 19, 2019.
Wafanyakazi wa Stesheni ya Fuga wakishuhudia uwezo wa mtambo aina ya Raech Stacker wa kunyanyua mizigo mizito katika stesheni ya Fuga uliozinduliwa jana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye, akitelemka kutoka kwenye moja ya mtambo wa kunyanyulia mizigo mara maada ya kuuzindua hapo jana katika Stesheni ya Fuga itayotumika kopokea na kusafirisha mizigo kwenda mradi wa Umeme JN HPP.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye, akipata maelezo fulani kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya usambazazi mitambo ya kunyanyulia mizigo ya Eristic (t) Investment Company, Hassan Kipussi katika uzinduzi wa mitambo hiyo uliofanyika katika Stesheni ya Fuga jana Agosti 19, 2019.
(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)
No comments:
Post a Comment