Rais Mstaafu Awamu ya
Tatu, Tanzania Mhe. Benjamin Mkapa, akihutubia katika Mhadhara wa Viongozi na
Wajumbe wa SADC, uliofanyika leo katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam.
Jumuiya ya Maendeleo
ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) inatakiwa kukumbuka na kurejea kwenye Dira
na Dhima za Jumuiya hiyo ili kuweza kuimarisha, kuongeza na kuwezesha ushirikiano
wa nchi za kusini mwa Afrika kuwa katika lengo moja na kusonga.
Hayo yalisemwa na
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Tanzania Mhe. Benjamin Mkapa alipokuwa
akizungumza leo katika mhadhara wa wajumbe na viongozi wa SADC katika Maktaba
ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Rais Mkapa alisema
kuwa katika kujenga uchumi ulioimara nchi hizo zinatakiwa kukumbuka Dira na
Dhima ya kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ya nchi za Kusini mwa Afrika ili kuweza
kuimarisha uchumi ulioendelevu; wenye kuwezesha wananchi kutoka nchi wanachma
kuwa na maisha bora.
“Naamini kuwa SADC imeweza
kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye muundo wa Maendeleo ya Bara la Afrika, na
suala hili linapaswa kutangazwa ili ushirikiano huu uendelee kwa wananchi
wanachama wa SADC, lakini haya yote yamesababishwa na kuwa na Dira na Dhima
ambayo inaruhusu nchi hizi kuwaza na kutekeleza mawazo yao pamoja”, alisema
Mkapa.
Kiongozi huyo Mstaafu
alisema kuwa SADC inatakiwa kukumbuka Dira ya kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo
ambayo ni kuunganisha na kuhusianisha Utumiaji wa rasrimali zilizoko nchi
wanachama ili kuwezesha nchi hizo kujitegemea na kuimarisha uchumi wake pamoja
na maisha ya watu wake.
Mkapa alifafanua kuwa
Dira hiyo inapaswa kutekelezwa huku nchi wanachama wakikumbuka waasisi wa SADC
akiwemo Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere kuwa ilikuwa ni kuungana nakufanya
kazi kwa pamoja ili kulinda rasrimali na kuwezesha wananchi kujitegemea kwa
kuisha maisha yaliyobora.
Aidha, Mkapa alisema
kuwa SADC ina dhima kubwa ya kuendeleza uchumi endelevu na ulio sawa kwa nchi
wanachama kupitia mifumo mizuri, utawala bora na kuongeza ushirikiano wa nchi
hizo, na vitu hivyo vitawezesha upatikanaji wa amani na usalama kwa nchi
wanachama pamoja na ujenzi wa miradi mbalimbali ya ushirikiano.
“Dira ya SADC ni moja
na nguzo muhimu katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ikiwemo miradi ya
Nishati, Miundombinu ya usafarishaji na ujenzi wa viwanda hii yote ni
utekelezaji wa kuifanya SADC kuwa katika uchumi ulio sawa ukanda huu wa nchi za
kusini mwa Afrika”, alisema
Aliongeza kuwa
Miundombinu ya nchi za Afrika inatakiwa kuimarishwa kama mkakati wa nchi za
SADC unavyoeleza, kwa sasa SADC inatakiwa ijikite katika ujenzi wa Viwanda na Nishati
ambapo vitu hivyo vikitekelezwa SADC itasonga mbele.
Kwa upande wake Naibu
Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Namibia, Natumbo Nandi
Ndaitwah, alisema kuwa Jumuiya ya SADC inapaswa kuzingatia kumbukumbu ya
kuasisiwa kwake ili kuweza kusonga mbele katika mashirikiano ya pamoja kwa nchi
hizi.
Waziri Ndaitwah alisema
kuwa kumbukumbu ya Waasisi wa SADC itakumbukwa milele huku akiitaja Tanzania
kuwa ni moja ya Taifa ambalo limeweza kusaidiwa kwa kiasi kikubwa katika
ukombozi wa Afrika na kundwa kwa jumuiya hiyo.
“Nchi wanachama wa SADC
tunapaswa kujua kuwa Tanzania ni taifa ambalo limewezesha kwa kiasi kikubwa kuzaliwa kwa Jumuiya hii,
kwani Mwl. Nyerere aliwezesha nchi nyingi za upande wa Kusini mwa Afrika
kukombolewa na alikuja na wazo la kuunda Jumuiya ya SADC ili nchi za kusini
zipate kufanya kazi pamoja na kuimarisha maisha ya watu wao”, Naibu Waziri
Mkuu, Ndaitwah.
Waziri Ndaitwa
alisema kuwa Mwl.Nyerere ni mfano wa kuigwa kwa nchi wanachama wa SADC na anapaswa
kubaki katika kumbukumbu ili vizazi vijavyo viweze kukumbuka kuwa kuna Mwanzilishi
na mkombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika.
“Namshukuru Baba wa
Taifa, Mwl.Julius Nyerere, aliyetangaza kuwa, Tanzania haiwezi kuwa huru kama Bara
la Afrika halijakombolewa, nayasema haya ili tujue tulikotoka na nani alifanya
kitu gani ili tuweze kusonga mbele katika Jumuiya hii ya Nchi za Kusini mwa
Afrika”, Naibu Waziri Mkuu, Ndaitwah.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe akitoa neno la utangulizi
katika Muhadhara, unaohusu masuala ya Kuongeza Ushirikiano kwa Nchi za Kusini
mwa Afrika ulifanyika leo Agosti 15, 2019 katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam.
Baadhi ya Washiriki
wa Muhadhara wa SADC, unaohusu masuala ya Kuongeza Ushirikiano kwa Nchi za
Kusini mwa Afrika wakifuatilia hotuba ya Rais Mstaafu Awamu ya Tatu, Tanzania
Mhe, Muhadhara huo ulifanyika leo Agosti 15, 2019 katika maktaba ya Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki
wa Muhadhara wa SADC, unaohusu masuala ya Kuongeza Ushirikiano kwa Nchi za
Kusini mwa Afrika wakifuatilia hotuba ya Rais Mstaafu Awamu ya Tatu, Tanzania
Mhe, Muhadhara huo ulifanyika leo Agosti 15, 2019 katika maktaba ya Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam.
Rais Mstaafu Awamu ya
Tatu, Tanzania Mhe, akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi kutoka nchi
mbalimbali na Viongzi wa SADC, mara baada ya muhadhara uliofanyika leo Agosti 15, 2019 katika maktaba ya Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam.
Rais Mstaafu Awamu ya
Tatu, Tanzania Mhe, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali ya
Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
na Viongzi wa SADC, mara baada ya muhadhara uliofanyika leo Agosti 15, 2019 katika maktaba ya Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam.
(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)
No comments:
Post a Comment