Ofisa Mafunzo Kitengo cha Masoko wa Kampuni ya Uwekezaji UTT-AMIS, Waziri Ramadhan, akitoa elimu ya Uwekezaji wa Pamoja kwa wafanyabiashara ndogondogo na vijana, eneo la Ilala, jijini Dar es Salaam.
Na.Mwandishi Wetu
OKTOBA 14, mwaka huu, Tanzania imeadhimisha miaka 20
ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Nyerere. Katika uhai wake, Mwalimu Nyerere alikuwa na sifa
ya utu, mpenda maendeleo, hakupenda kuona watu wakinyanyaswa, wakionewa au
kupuuzwa kwa sababu za unyonge wao.
Mwalimu Nyerere alichukia rushwa, ufisadi, wizi na
aina zote, kujenga misingi imara ya kulifanya Taifa lijitegemea, kutumi
rasilimali zilizopo ili kujiletea maendeleo ya kweli.
Pia Mwalimu Nyerere alipenda kuona taasisi
zilizoanzishwa na serikali zikiwakomboa Watanzania katika nyanja mbalimbali ili
waweze kukuza mitaji, kipato chao na kulipa kodi stahiki.Miongoni mwa taasisi iliyobeba maono ya Mwalimu
Nyerere na kuyafanyia kazi kwa vitendo ni UTT AMIS.
Taasisi hiyo ipo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango
iliyopewa dhamana ya usimamizi wa mali kupitia Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja.
Utajiri siyo fedha ambazo mtu anakusanya bali ni
fedha zinazowekwa na kufanya kazi. Tamaduni zetu zimeifanya jamii kubwa
kuhifadhi fedha ndani katika vyungu, magodoro, vibubu.
Uwekaji akiba na uwekezaji ni dhana mbili tofauti.
Uwekaji akiba ni mzuri lakini bila kuziwekeza ni bure.
Ili uwe muwekaji akiba mzuri, unapaswa kuwa na
nidhamu ya kujizoesha muda mrefu.
Awali UTT AMIS ilipewa dhamana ya usimamizi wa
mifuko mitano ambayo ni Mfuko wa Umoja, Wekeza Maisha, Watoto, Mfuko wa
Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi. Hivi sasa taasisi hiyo imeongeza mfuko mwingine wa
Hati Fungani.
Nchini Tanzania unaweza kuwekeza fedha zako katika
masoko ya fedha, mitaji. Hatua hiyo inahusisha akaunti za muda maalum na zisizo
za muda maalum katika benki za biashara.
Pia hati fungani za Serikali za muda mfupi, mrefu,
kampuni na hisa zilizoorodhosgwa katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) ambazo
zina nafasi kubwa ya kurejesha gawio zuri.
Uwekezaji unaofanywa na taasisi hiyo kupitia mifuko
ambayo wanaisimamia ni fursa mbadala inayowezasha watu, vikundi, taasisi,
kampuni kuwekeza pesa zao kwa Meneja wa UTT.
Meneja huzichukua fedha hizo, kuziwekeza kwenye
masoko ya fedha, mitaji kulingana na waraka wa makubaliano.
Faida inayopatikana hugawanywa kwa wawekezaji
kulingana na uwiano wa uwekezaji uliofanyika kwenye mfuko husika.
Mfuko wa Umoja, ulioanzishwa Mei 16, 2005 ukilenga
kutimiza mahitaji tofauti ya wawekezaji. Awali bei ya kipande ilikuwa sh. 70,
kwa sasa sh. 590.2060.
Sifa zilizopo katika mfuko huo ni vipande kuuzwa kwa
thamani halisi (hakuna gharama za kujiunga). kiwango cha chini cha kujiunga ni
vipande 10 tu.
Malipo ya mauzo hutozwa asilimia moja ya thamani
halisi, pia ni rahisi kujiunga, kutoka ambapo manunuzi na mauzo hufanyika kila
siku ya kazi.
Mfuko wa Watoto una lengo la kuwasaidia watoto
katika maendeleo yao nchini. Awali bei ya kipande ilikuwa sh. 100, mfuko
ulianzishwa Oktoba 1, 2008.
Sifa za mfuko huo ni uwekezaji kwa ajili ya mtoto
mwenye umri chini ya miaka 18. Kiwango cha chini cha uwekezaji sh. 10,000,
unaruhusiwa kuwekeza kidogo kidogo kwa sh. 5,000.
Sifa nyingine ni vipande kuuzwa kwa thamani halisi
(hakuna gharama za kujiunga), mfuko hutoa mipango ya aina mbili, kwanza malipo
ya ada, pili mpango wa kukuza mtaji.
Malipo ya ada na mauzo ya vipande yanaruhusiwa pale
mtoto anapofikisha miaka 12. Mfuko huo ni miongoni mwa mifuko inayotatua changamoto za kielimu hasa katika
ulipaji ada kwa wanafunzi, kutoa mtaji baada ya ukomo wa shule kufikia.
Pia mfuko una mipango miwili mikubwa, mpango wa ada
za shule na mtaji kwa mwanao. Ili mzazi aweze kuchangia kupitia mfuko huo,
anapaswa kuweka sh. 10,000 kima cha chini na hakuna ukomo kwenye kiwango cha
juu.
Mfuko ulianzishwa mwaka 2008.Kiwango cha chini cha
kipande kilianzia sh. 100, hivi sasa sh. 346.3151.
Mfuko wa Jikimu una lengo la kukidhi mahitaji ya
wawekezaji wanaohitaji uhakika wa mapato ya mara kwa mara, ulianzishwa Novemba 3, 2008 ukiwa na sifa za mipango ya
uwekezaji, kiwango cha uwekezaji, mpango wa gawio robo mwaka.
Kiwango cha chini cha uwekezaji sh. milioni 2,
mpango wa gawio wa mwaka (kiwango cha chini cha uwekezaji sh. milioni moja),
tatu mpango wa mwaka wa kukua (sh. 5,000).Vipande vinauzwa kwa thamani halisi
(hakuna gharama za kujiunga).
Mfuko wa Ukwasi unaotoa nafasi ya uwekezaji mbadala
kwa wawekezaji wakubwa au taasisi ambao wangependa kuwekeza fedha zao za ziada
kwa kipindi kifupi ama cha kati huku wakikuza mtaji wao.
Ulianzishwa Aprili 30, 2013, bei ya kipande ikiwa
sh. 100.00, hivi sasa imepanda sh. 126.3239.
Sifa za mfuko huo ni rahisi mwekezaji kupata fedha
zake za mauzo ya vipande ndani ya siku tatu za kazi baada ya maombi ya kuuza
vipande kupokelewa Makao Makuu ya UTT AMIS.
Mfuko huo hauna ada ya kujitoa wala kujiunga, una
unafuu wa gharama za uwekezaji, unafaa kwa wawekezaji mmoja mmoja au taasisi,
kiwago cha chini cha kuwekeza sh. 5,000,000.00.
Kuongeza uwekezaji wako sh. 1,000,000.00, pia
unaruhusu uhamishaji vipande kutoka kwa mwekezaji mmoja kwenda mwingine,
kuruhuusu uhamishaji vipande kwenda kwenye mifuko mingine, kuviuza kwa thamani
halisi.
Mfuko wa Wekeza Maisha unamwezesha mwekezaji kupata
faida pacha (mapato mazuri pamoja na mafao ya bima).
Mfuko huo ulianzishwa Mei 16,2007, wawekezaji kati
ya miaka 18 na 55 ndio wanaoruhusiwa kujiunga. Unatoa mipango ya aina mbili,
kuchangia uwekezaji awamu ya kwanza, mkupuo mmoja.
Vipande vinauzwa kwa thamani halisi, hakuna gharama
za kujiunga. Kujiunga ni sh. 8,340.00 tu kwa mwezi. Bei ya kipande kwa sasa sh.
416.4499. Mafao ya bima yanayopatikana ni bima ya maisha,
ulemavu wa kudumu na bima ya ajali.
Mfuko unamwezesha mwekezaji kuwekeza kwa mpangilio,
kuchangia kwa mwezi, mara mbili kwa mwaka, mara moja kwa mwaka ambapo faida za
uwekezaji katika Mifukoya Uwekezaji wa Pamoja ni kukuza mtaji kwa kutoa faida
nzuri ukilinganisha na mifuko mingine kwenye masoko ya fedha.
Faida nyingine ni kutawanya hatari za uwekezaji,
mwekezaji hupunguza athari za uwekezaji kwa kuwekeza katika uwekezaji auai,
wawekezaji kufaidika na unafuu wa gharama za uwekezaji.
Pia wawekezaji wanaweza kufuatilia maendeleo ya
masoko ya fedha kwa kufuatilia maendeleo ya mifuko.
Mfuko mpya Hati Fungani unaojulikana kama ‘Bond
Fund’ ni kati ya mifuko ya uwekezaji wa pamoja inayoendeshwa na UTT AMIS
ulioanzishwa kwa malengo maalum.
Kuanzishwa kwa Mfuko wa Hati Fungani kumetokana na
mahitaji ya wawekezaji na uchambuzi wa bidhaa za kifedha zilizoko kwenye soko
la mitaji kwa sasa.
Mfuko utawawezesha wawekezaji wadogo na wa kati
kuzifikia fursa za uwekezaji ambazo kwa hali ya kawaida ni wawekezaji wachache
na wakubwa ndio wanaozifikia.
Pia utawekeza kwenye hati fungani zilizoorodheshwa
kwenye soko la hisa kwa asilimia 90 na asilimia 10 itakuwa kwenye uwekezaji
wenye ukwasi mkubwa.
Lengo ni kuwawezesha wawekezaji wanaohitaji kuchukua
fedha kutokana na uwekezaji wao katika mfuko wafanye hivyo.
Mfuko umeundwa ili kumwezesha kila mwekezaji
kuchagua kama anapenda kukuza mtaji au kupokea gawio kwa mwezi, kila miezi sita
kutokana na mahitaji yake ya kifedha.
Akiuzungumzia mfuko huo, Mkurugenzi wa Masoko na
Uhusiano wa UTT AMIS, Daudi Mbaga, alisemaumelenga kuondoa changamoto ambazo wawekezaji
wanakutana nazo.
Anasema soko la fedha lina bidhaa nyingi
zilizobuniwa ili kukidhi mahitaji tofauti ya watumiaji.
Baadhi ya bidhaa hizo zinaeleweka kirahisi hata
namna ya kuzifikia na kuwekeza lakijni wakati mwingine hazitoi faida shindani
kwa wawekezaji.
Anasema baadhi ya wawekezaji hasa wadogo ni vigumu
kuwekeza kwenye baadhi ya bidhaa katika soko la fedha. Mfuko wa Hati Fungani
umeratibiwa ili kuondoa changamoto hizo.
Mwekezaji anapata faida sawa na wawekezaji wakubwa,
akihitaji fedha anauza baadhi ya umiliki wake kwenye mfuko kwa utaratibu rahisi
bila kupoteza faida aliyoipata.
Pia mfuko huo unawafaa wawekezaji wakubwa kwa sababu
ya faida shindani, gharama ndogo za kuwekeza, ukwasi wa kutosha, usalama wa
mtaji, hatari ndogo za uwekezaji.
Mfuko unatoa fursa kwa wawekezaji kuwekeza,
kushiriki katika masoko ya mitaji, kufaidika na uwekezaji huo.
Kwa mantiki hiyo, mfuko umeandaliwa ili kutoa fursa
kwa wawekezaji wa kipato cha chini, kati na kipato cha juu ambao ni watu
binafsi, kampuni, taasisi na vikundi rasmi wanaweza kushiriki katika uwekezaji
kwenye mfuko huo.
Mbaga anasema, mfuko una mipango miwili ya uwekezaji
ili kukidhi matakwa tofauti ya wawekezaji.
Kuna mpango wa kukuza mtaji, gawio kila mwezi na
gawio kila miezi sita, mpango wa kukuza mtaji.
Gawio la mara
kwa mara halitatolewa kwa wawekezaji badala yake faida iliyopatikana
itarudishwa kwenye uwekezaji wa awali kwa kununua vipande vitakavyonunuliwa kwa
bei ya wakati huo.
Mpango huo utawafaa wawekezaji wanaohitaji kuweka
akiba kwa malengo maalum mfano kujenga nyumba au wafanyakazi wenye kipato kama
wangependa kuwa na fedha ya akiba.
Wawekezaji katika mpango huo wanaweza kuuza kiasi
chochote cha uwekezaji wakiwa wamekidhi vigezo vinavyohusu uuzwaji wa
vipande.
Wawekezaji wanaohitaji kuchukua
faida kila mwezi kama wastaafu wanaopata
fedha zao za mkupuo, kuwekeza kwenye mfuko, wanashauriwa kuchagua kupokea gawio
kila mwezi ili wapate kipato cha kuishi bila kupoteza fedha walizopata.
Mbaga anasema wawekezaji wengine wanaopata fedha
nyingi mara moja mfano wachimba madini, wanaweza kuchagua gawio kila mwezi ili
wafanye shughuli zao bila kuathiri mtaji wao.
Pia wawekezaji watakaojiunga na mpango huo wanaweza
kuuza vipande kidogo au vyote ili mradi wawe wamekidhi vigezo vya mfuko
vinavyohusu uuzwaji vipande.
Mpango wa gawio kila miezi sita, Mbaga alisema hutegemea na mahitaji ya fedha ya
mwekezaji na anavyochagua kwenye fomu ya maombi ya kuwekeza kwenye mfuko.
Kwa wawekezaji ambao wanahitaji kuchukua faida kila
miezi sita mfano wafanyakazi wanaohitaji kuweka kiasi cha fedha ili faida
inayopatikana itumike kulipa ada kusomesha watoto, wanaweza kuchagua kupokea
gawio kila miezi sita.
Pia kuna wawekezaji wanaopata fedha nyingi mara moja
kama wakulima wa mazao mbalimbali ya msimu, wanaweza kuchagua kupata gawio kila
miezi sita.
Wawekezaji watakaojiunga na mpango huo wanaweza
kuuza vipande kidogo au vipande vyote ili mradi wawe wamekidhi vigezo vya
mfuko.
No comments:
Post a Comment