Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU e.V umefanya mkutano mkuu wa uchaguzi mjini Aschaffenburg Ujerumani jumamosi 28.09.19. Katika uchaguzi huo watanzania wanaoishi ujerumani walichagua viongozi wapya, nafasi ya mwenyekiti alichaguliwa Mwl. Bi Upendo Vanessa Lyimo Foelesen kuwa mwenyekiti wa UTU e.V, baada ya mwenyekiti mstaafu Bw. Mfundo Peter Mfundo kukataa kugombea nafasi hio, ambayo amekaa kwa muda wa miaka 9, na kukitumikia chama hicho kwa muda wote huo, hata hivyo kamati ilimuomba achukue nafasi ya heshima kuwa mwanakamati, mshauri, mlezi wa UTU e.V na kiongozi muandamizi katika shughuli za UTU e.V
Watanzania wanaoishi ujerumani waliwachagua viongozi wafuatao.
Mwenyekiti: Mwl. Bi Upendo Vanessa Lymo
Makamo Mwenyekiti: Bw. Malumbo Salim Malumbo
Katibu: Bi. Petrida Karch
Muweka hazina: Bw. Mngoya Lukuta
Wanakamati:
Bw. Mfundo Peter Mfundo
Bw. Ebrahim Makunja (aka Kamanda Ras Makunja)
Bw. Sudi Mnette
No comments:
Post a Comment