Habari za Punde

OMBI LA KUPATIWA MSAADA KWA AJILI YA KUPANUA MSIKITI PAMOJA NA MADRASA (CHUO)
Uongozi wa masjid ikhlasw uliopo shaurimoyo Zanzibar tayari umepanga kuleta maombi kwenu waislamu kwa lengo la kupanua msikiti pamoja na madrasa (chuo) kwa lengo la kuendesha dini ya Allah (s.w) mbele.

Hatua hii ya kupatiwa jengo la msikiti pamoja na chuo itapelekea kuweza kupata nafasi nzuri ili tuweze kuwasomesha watoto wetu, watu wazima, pamoja na jamii kwa ujumla, kama alivosema Allah (s.w)... “na toeni vile alivokupeni m/mungu kabla hayajamfika mmoja wenu mauti……. Suratu- almunafiqoon. “10”

Kwa kuzingatia hilo basi tunawaomba waislamu wote hususan wale ambao allah kawajaalia kuwa na mali waitumie fursa hii kwani kujenga msikiti ni moja kati ya alama kubwa sana ambazo Allah amezisifia, kama alivosema Allah (s.w)
“hakika sivyenginevyo isipokuwa wale wenye kusimamia Misikiti ya Allah ni wale waliomuamini Allah na siku ya mwisho” Attauba “18”

Na akasema tena mtume Muhammad (s.a.w) ….
“mwenye kujenga msikiti mmoja hapa duniani Allah atamjengea nyumba peponi”

Tunategemea maombi yetu haya yatakuwa ni yenye kuzingatiwa na kufanyiwa kazi.

Tunamuomba Allah atufanyie wepesi juu ya jambo hili.

MASJID IKHLASW

PBZ A/C NO             0738694001

M'PESA A/C NO       0747656537

TIGO PESA A/C NO    0672519303   

WABILAH TAUFIQ

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.