Habari za Punde

Serikali itaendelea kuwalinda na kuwathamini wazee

Na Bahati Habibu          Maelezo  

Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar  imesema itaendelea   inawalinda na kuwathamini Wazee kwani wao ndio waliofanya kazi kubwa ya kupigania uhuru na kuuondosha utawala wa kidhalimu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi ,Mawasiliano na Usafirishaji Dkt Sira Ubwa Mamboya katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa jengo la makaazi ya wazee Sebleni ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra ya kutimiza miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Amesema Serekali ya awamu ya kwanza chini ya uongozi wa Marehemu Mzee Abeid Amani Karume alijenga makaazi ya wazee ili na wao kuwa na furaha ya maisha baada ya kufanya kazi ngumu ya kuiletea maendeleo Zanzinbar.
’’ Wazee ni chachu ya kuleta maendeleo kwa Taifa lolote duniani kutokana na busara na hekima zao hivyo yafaa kutunzwa na kuangaliwa kwa jicho la tatu ili kuitumia hadhina waliyo nayo.’’ Alisema Waziri huyo.
Aidha amempongeza Rais wa  Zanzibar na Mwenyekititi wa Baraza la Mapinduzi. Dkt Ali Muhamed Shein kwa kuendeleza yale yote yalioazishwa na Serekali ya awamu ya kwanza kwa kuimarisha  Miondombinu iliyo bora, Afya na  Elimu .
Na kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi Uwezeshaji , Wazee ,Wanawake na Watoto. Fatma Gharib Bilali amesema lengo la Serikali kuendelea kukarabati majengo yaliyo chakaa ni kuhakikisha yanakarabatiwa na kuwa na haiba nzuri kama aliyo iwacha marehemu Mzee Abeid Amani Karume .
Zaidi ya shilingi milioni mia tatu ishirini zimetumika kukarabati jengo la makazi ya Wazee ambalo sehemu ya chini ya jengo hilo litatumika kwa shughuli za Kiofisi kwa Wizara ya Kazi , Uwezeshaji , Wazee , Wanawake na Watoto na sehemu ya juu itakuwa ni skuli  itakayofundisha  mafunzo ya Sheria.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.