Habari za Punde

PSSSF KUTOA HUDUMA KAMILI ZA KIOFISI MAONESHO YA 44 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM

Afisa Mafao PSSSF, Bw. Abdallah Juma Adam (kushoto), akimuhudumia mwanachama wa PSSSF aliyefika kwenye banda la Mfuko huo, Julai 2, 2020.

Na.Mwandishi Wetu Dar-es-Salaam.                                            
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umesema katika msimu huu wa maonesho ya 44 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam unatoa huduma kamili kama ambazo zinazopatikana kwenye ofisi zake kote nchini.

Akizungumza na  kwenye banda namba 13 la Mfuko huo kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu kama Sabasaba, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam , Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF Bw. Abdul Njaidi amesema kwa mantiki hiyo Mfuko umewaalika wanachama wa Mfuko na wananchi kwa ujumla kufika katika banda hilo ili kujipatia huduma na taarifa mbalimbali.

“Tunawakaribisha wanachama wetu na wananchi kwa ujumla kutembeela banda letu kwani huduma zote za kiofisi ambazo zinapatikana kwenye ofisi zetu zilizoenea kote nchini zinapatikana hapa.” Alisema Bw. Abdul Njaidi.

Alitaja huduma hizo kuwa ni pamoja na mwanachama kupata taarifa kuhusu Pensheni, Mafao, uhakiki, uwekezaji na taarifa za michango.

Katika hatua nyingine, Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Uendelezaji Bishara Tanzania (TANTRADE), Bi. Theresa Chilambo amesema Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa anatarajiwa kuyafungua rasmi maonesho hayo  Ijumaa Julai 3, 2020.
 Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF Bw. Abdul Njaidi (wakwanza kushoto), akimsikiliza mwananchi huyu aliyetembelea katika banda la PSSSF leo Julai 2, 2020. Katikati ni Bw. Meseka Kadala, Afisa Uhusiano wa Mfuko huo.
 Afisa Matekelezo Mwandamizi wa PSSSF, Bw.Donald Maeda (kushoto), akimsikiliza mwanachama wa Mfuko aliyefika kwenye banda la PSSSF ili kupata taarifa za michango yake.
 Wanachama wa PSSSF wakihudumiwa kwenye banda la Mfuko huo LEO jULAI 2, 2020.
 Afisa Huduma kwa kwa wateja mwandamizi wa PSSSF, Bi. Nelusigwa Mwalugaja (kulia) akimuhudumia mwanachama wa Mfuko huo Julai 2, 2020.
  Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF Bw. Abdul Njaidi (wakwanza kushoto) na Afisa Uhusiano wa Mfuko huo Bw. Meseka Kadala, wakiwasikiliza wananchi hawa waliohitaji kuhudumiwa Julai 2, 2020.
Afisa Mafao PSSSF, Bw. Abdallah Juma Adam (kushoto), akimuhudumia mwanachama wa PSSSF aliyefika kwenye banda la Mfuko huo, Julai 2, 2020.
Afisa Matekelezo Mwanzamizi wa PSSSF, Bi. Zainab Ndullah (kulia), akimuhudumia mwanachama wa Mfuko huo Julai 2, 2020.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.