Habari za Punde

Innaa Lillaahi wainnaa ilayhi Raajiuun: Mzee Hassan Nassor Moyo ametangulia mbele ya haki

Marehemu Mzee Hassan Nassor Moyo enzi za uhai wake

Na Hamida Kamchalla, TANGA
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar ambaye aliwakutanisha aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF Maalim Sief Shariff Hamadi na Rais wa Awamu ya Sita ya SMZ Amani Abaedi Karume ,Hassan Nassoro Moyo(87)amefariki usiku wa kuamkia jana Jumanne  katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga,Bombo jijini hapa baada ya kuugua ghafla majira ya saa 5 usiku wa Jumatatu.

Kwa mujibu wa mtoto wa pili wa marehemu,Mohamedi Moyo ambaye ni Katibu wa CCM wilayani Muheza amesema kuwa marehemu mzee Moyo amefariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali baada ya kuhisi kubanwa kifua na kukosa pumzi.
Amesema kuwa,marehemu kutwa nzima ya siku ya Jumatatu marehemu mzee  Moyo alishinda vizuri nyumbani kwake ilipofika usiku ghafla alijisikia kifua kubana na kukosa pumzi ndipo mkewe akaamua kumpeleka hospitali ya rufaa ya Bombo ambayo ni jirani na nyumbani kwake maeneo ya Mtaa wa Bombo na Raskazone.
“Jana(juzi)kutwa nzima mzee alikuwa anaendelea vizuri,ilipofika usiku wa kati ya saa 5 na saa 6 usiku kifua kikaanza kumbana akwa hapati pumzi vizuri ndipo bi mkubwa(mama) akaamua kumpeleka hospitali kufika kule baada ya vipimo akawekewa mashine ya kusaidia kupumua,haikuchukua hata nusu saa akafariki dunia,”alisema.
Aliongeza, “kwa mujibu wa taarifa za madaktari marehemu alikuwa anasumbuliwa na tatizo la ‘Cardiac Respiratory Arrest’.
Baada ya kufariki jana(Jumanne)majira ya saa 3:45 asubuhi mwili wa marehemu ulisafirishwa kwa ndege kuelekea Fuoni Zanzibar kwa ajili ya maiko.
Kwa mujibu wa Mohamedi Moyo,marehemu ameacha wake wawili,watoto 15 na wajukuu zaidi ya 60.
WASIFU
1964:Hassan Nassoro Moyo alikuwa Waziri wa Kwanza wa Katiba na Sheria katika Serikali ya kwanza  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Amekuwa Waziri wa Elimu,Kilimo na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi katika serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ).
1965 -1995 Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano,Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM kuanzia mwaka 1977 hadi 1997.
Alikuwa miongoni mwa wajumbe 10 kutoka Zanzibar waliounda Chama cha Mapinduzi CCM na alikuwa Katibu wa Mipango wa Chama cha Afro Shiraz Party(ASP).
Mzee Hassan Nassoro Moyo anakuwa Waziri wa mwisho wa Nyerere kufariki na alitumikia nafasi ya Uwaziri katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuanzia Rais Abeid Amani Karume hadi Rais Abdu Jumbe Mwinyi na kwa upande wa Jamhuri ya Muungano ametumikia nafasi hiyo katika serikali ya awamu ya kwanza na ya pili.
Ndege iliyobeba maiti ya Mzee Hassan Nassor Moyo ikiwa tayari kuupakia mwili wa Mzee Hassan Nassor Moyo aliefarika Tanga jana saa saba za usiku
Baadhi ya wanafamilia ya Marehemu Hassan Nassoro Moyo wakipanda katika ndege baada ya kupakiwa mwili wa marehemu kuelekea Zanzibar kwa ajili ya maziko yanayofanyika katika Kijiji cha Fuoni Wilaya ya Magharibiu "A" Unguja, marehemu amefariki Mkoani Tanga jana usiku.
Ndugu na jamaa wa marehemu Mzee Hassan Nassor Moya wakiwa katika uwanja wa ndege Tanga baada ya kuupakia mwili wa marehemu katika ndege ya kukodi kwa ajili ya kusafirishwa Zanzibar kwa maziko yanayotarajiwa kufanyika katika Kijiji cha Fuoni Wilaya ya Magharibi "A" Unguja baada ya sala ya Alasiri katika msikiti wa Waraab Fuoni,
Marehemu amefariki Mkoani Tanga na kusafirishwa leo kuelekea Zanzibar nyumbani kwake fuoni.
Tumuombe Allaah Subhaanahu wata'ala amsamehe makosa yake na ampe kauli thabiti na aijaalie pepo iwe ndio makaazi yake. Allaahumma Amin

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.