Habari za Punde

Makamu wa Rais Mhe Samia ahudhuria kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kilichokutana leo Dodoma

\


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Halmashauri kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia suluhu Hassan, leo Agosti 18,2020 ameshiriki katika kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kilichokutana Ikulu Chamwi
 Baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya Halmashauri kuu ya  CCM Taifa wakiwa katika kikao cha kamati hiyo , Ikulu Chamwino Dodoma leo
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Halmashauri kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiteta jambo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kulia na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid kushoto kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kilichokutana leo Agosti 18,2020 Ikulu Chamwino Dodoma.  
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Halmashauri kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM na Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kilichokutana leo Agosti 18,2020 Ikulu Chamwino Dodoma.  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.