Habari za Punde

MKURUGENZI MKUU TBS AIFAGILIA WIZARA YA AFYA –IDARA KUU YA MAENDELEO YA JAMII

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango nchini, TBS Dkt.Athuman Ngenya (kulia) akiangalia majarida na vitabu mbalimbali vya miongozo inayotokewa na Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii wakati aipotembelea banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya Nanenanekatika viwanja vya Nyakabindi, Simiyu kushoto ni Afisa Ustawi wa Jamii Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Loata Mollel.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Erasto Ching’oro akitoa maelezo kwa mwananchi aliyetembelea banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Nyakabindi, Simiyu.
Na Mwandishi Wetu Simiyu
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango nchini, TBS Dkt. Athuman Ngenya ameipongeza Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii kwa huduma bora kwa walengwa hasa wanawake na wananchi wa kipato cha chini.

Dkt. Ngenya ameyasema hayo katika Viwanja vya Nyakabindi, Simiyu baada ya kushuhudia huduma zinazotolewa na Wizara hiyo kwa walengwa.

Mkurugenzi huyo wa TBS ameeleza kuvutiwa huduma zinazotolewa na Wizara ili kuwawezesha walengwa hasa Wanawake na watu wenye hali ya chini.

“Nimevutiwa sana na huduma zenu kwa jamii mkishirikiana na TAMISEMI mtaweza kuwasaidia wajasriamali yakiwemo kuwawezesha kiuchumi" alisema.

Ameongeza kuwa TBS kwa upande wake ina inaendesha program maalum ya kuwawezesha wanawake kujiwezesha kiuchumi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.