WAFANYABIASHARA wanawake Kisiwani Pemba, wakiwa
katika kikao cha pamoja cha kuwasilisha katiba ya Jumuiya ya wafanyabiashara
wanawake Zanzibar, kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Makonyo Wawi mjini
Chake Chake.(PICHA NA ABDI
SULEIMAN,PEMBA)
MKUU wa Wilaya ya Micheweni Salama Mbarouk Khatib,
akiwasalimia wafanyabiashara wanawake Kisiwnai Pemba, mara baada ya kuwasili
katika ukumbi wa Mkonyo, kwenye kikao cha kuwasilisha katiba ya jumuiya ya
wafanyabiashara wanawake Zanzibar.(PICHA
NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)
KATIBU wa Muda wa Jumuiya ya Wafanyabiashara
Wanawake Zanzibar Fatma Mabrouk Khamis akiwasilisha mabadiliko yaliyofanyiwa
katiba ya jumuiya hiyo, katika kikao cha pamoja na wafanyabiashara wanawake
Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI
SULEIMAN,PEMBA)
MWANASHERIA Naima Mwinzagu akiwasilisha baadhi ya
vipengele vya sheria ya Jumuiya ya wafanyabiashara wanawake Zanzibar, katika
kikao cha pamoja na wafanyabiashara wanawake Kisiwani Pemba huko Makonyo Wawi.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)
AFISA Mdhamini Wizara ya Biashara na Viwanda Pemba
Ali Suleiman Abeid, akizungumza jambo na baadhi ya wafanyabiashara wanawake wa
Pemba, wakati wa kuchagua wajumbe wanne mmoja kutoka kila Wilaya, ambao
watawakilisha katika kikao cha bodi ya jumuiya ya wafanyabiashara wanawake
Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)
No comments:
Post a Comment