. Waziri wa Utalii na
Mambo ya Kale Mhe Lela Muhamed Mussa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba
Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman wakisaini vitabu vya
kumbukumbu ya makabidhiano ya majukumu ya kiutendaji
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe Lela Muhamed Mussa akimkabidhi nyaraka muhimu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman .
Na RAYA HAMAD (OR- KSUUB)
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman amekabidhiwa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe Lela
Muhamed Mussa .
Mara baada ya
makabidhianao hayo Waziri Haroun amewaasa wafanyakazi kuwa waadilifu kwani
nyaraka zina thamani kubwa na kuahidi
kuimarisha zaidi taasisi hio hasa katika masuala ya kuweka kumbukumbu kwani ni
hazina muhimu kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na kuhakikisha
wafanyakazi wanapaiwta mafunzo mbalimbali pamoja na stahiki zao
Mhe Haroun amezuwia
kwa muda makubaliano yote
yaliyoihusisha Taasisi ya Nyaraka na kumbukumbu ili kujiridhisha juu ya
utaratibu uliotumika ameahidi kuimarisha
mashirikiano na wote wenye nia njema ya kuisaidia Zanzibar kwa njia ambazo ni za kheri isiwe
makubaliano ya kunufaisha upande mmoja ila yawe
yanazinanufaika pande zote kwa maslahi
ya taifa
‘Kuna nyaraka
zilizowahi kuibiwa na waliotoa ni wafanyakazi kutoka taasisi hii Serikali
ikachukuwa hatua kwa wale waliohusika lakini nasikitishwa sana kuona kumbe
maradhi haya hayajesha ‘
Aidha Mhe Haroun amekemea
tabia na mtindo uliozuka hivi sasa kwa baadhi ya wafanyakazi na watendaji wa
Serikali wasiowaaminifu kutoa siri za Serikali na kuzisambaza kupitia magurupu
mbali mbali ya mitandao ya kijamii jambo ambalo ni kinyume na maadili na
taratibu za kiutumishi
‘ kuanzia sasa
mfanyakazi yeyote wa Serikali tukimbaini na akijulikana anatoa siri za Serikali
hatua kali za kisheria zitachukuliwa naomba wafanyakazi na watendaji waelewe
kuwa tunafatilia kwa makini sana wale
wote wanaovujisha siri za Serikali na baadhi yao tayari tumeshawapata na
watachukuliwa hatuwa za kinidhamu’ alilisitiza
Nae Waziri wa Utalii
na Mambo ya Kale Mhe Lela Muhamed Mussa amesema nyaraka ni rasilimali muhimu na
inayohitaji kuangaliwa kwa umakini sana katika kipindi cha miaka mitano ambapo amemuomba Waziri Haroun kuangalia makubaliano yaliyofikiwa kati ya Taasisi ya
Nyaraka na Kumbukumbu ya Zanzibar na Taasisi nyengine zilizoingia makubaliano
hayo
Mhe Lela amekabidhi
taarifa ya utendaji kwa kipindi cha
miaka mitano, muundo wa taasisi na
vitengo mbalimbali, nakala za baadhi ya
nyaraka zilizowahi kuibiwa na kupatikana kutoka nchi mbali mbali pamoja na
nyaraka za makubaliano yaliyofikiwa na Taasisi hio
Aidha Mhe Lela
amemkabidhi Waziri Haroun Mkataba wa
makubaliano ya awali baina ya Idara ya Nyaraka na Makumbusho ya Zanzibar na
Makumbusho ya Taifa na Nyaraka ya Oman yaliyosainiwa Tarehe 30 April, 2020
Makubaliano ya
Makabidhiano ya Uhamishaji wa nyaraka baina ya Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya kale na Bi Saada Shaaban Shahdad,
Nyaraka ya fotokopi ya andiko binafsi la Mhe Salim Bin Nasser Al-Ismail ambayo
ameiwasilisha Idara ya Makumbusho na Nyaraka Zanzibar kwa madhumuni ya
kuhifadhiwa
Taasisi ya Nyaraka na
Kumbukumbu za Serikali ndio yenye dhamana ya kuzihifadhi na kuzitunza nyaraka
zote katika eneo salama hivyo nyaraka
zinazohusiana na maandishi zitaendelea
kuwa katika Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora na yale
yanayohusiana na mambo ya kale yakiwemo
makumbusho yataendelea kubakia kwa Wizara husika ambayo ni Wizara ya Utalii Mambo ya kale
Makabidhiano hayo
yalihudhuriwa na viongozi mbali mbali kutoka
Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora, Wizara ya Utalii
na Mambo ya Kale na wafanyakazi wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu katika
ukumbi wa taasisi hio Kilimani
No comments:
Post a Comment