Habari za Punde

Waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali awataka wauguzi kuandaa utaratibu kumwezesha mtoto Sabah Hamad kufanya mitihani yake

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar mhe Simai Mohammed Said akimjuulia hali mtoto Sabaha Hamad Juma aliyeunghuzwa mafuta ya moto na mama yake mzazi huko Kwarara mjini Unguja
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar mhe Simai Mohammed Said akizungumza na madaktari na wasimamizi ya wadi ya watoto alipofika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja jana
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar mhe Simai Mohammed Said akimfariji mtoto Sabaha Hamad Juma ambae aliunguzwa mafuta ya moto na mama yake mzazi huko Kwarara mjini Unguja.


Na Maulid Yussuf , WEMA 

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar mhe Simai Mohammed Said amewataka wauguzi wa Hospitali ya Mnazimoja kuhakikisha wanamfuatilia kwa karibu mtoto Sabaha Hamad Juma, juu ya matibabu yake ili aweze kuendelea na mitihani yake ya darasa la sita inayoanza kesho hapa Zanzibar.

Mhe Simai ameyasema hayo wakati alipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kumkagua baada ya kuunguzwa Mafuta ya moto na Mama yake Mzazi Huko Nyumbani kwao Kwarara na kuangalia namna ya kumsaidia Mtoto huyo kwa lengo la kuendelea na mitihani yake.
Amesema kutokana na mtoto huyo kudai mwenyewe juu ya kufanya mitihani yake, Mhe Simai amesema watashirikiana na Idara ya Ustawi wa jamii pamoja na wataalamu wa afya kuweka mbinu mbadala za kuweza kumpelekea usafiri ili aweze kufanya mitihani yake hiyo.
Mhe Simai ambae pia ni Kaimu Waziri wa Afya ametumia nafasi hiyo kwa kuwataka Madaktari pamoja na wauguzi kote nchini, kujitahidi katika kuwahudumia vizuri wagonjwa wanapofika Hospitali pamoja na kuwa wapole kwa kutegemea malipo kutoka kwa mola wao.
Nae Mkurugenzi Idara ya Ustawi wa jamii Bi. Wahida Maabadi Mohammed amesema anasikitishwa kwa mzazi wa mtoto huyo kwa kitendo alichokifanya ukizingatia kuwa na yeye pia ni mwalimu wa Skuli, hivyo amewaomba wazazi kutokuwa na hasira kwa watoto kwani hasira ni hasara.
Kwa upande wao wauguzi na madaktari wanaoshughulikia hali ya mtoto huyo, Dr. Msafiri Marijani wamesema kutokana na hali yake hivi sasa inaridhisha, lakini bado anahitaji mazoezi ya hali ya juu ili kumuepusha kupata ulemavu wa miguu kutokana na kuungua kwake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.