Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi Amefanya Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya Zanzibar.

                                                                    

STATE HOUSE ZANZIBAR

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE

Zanzibar02.01.2021

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyiamefanya mabadiliko kwenye uteuzi wa Wakuu wa Wilaya uliofanyika tarehe 28 Disemba, mwaka jana 2020.                                                                                    

Walioteuliwa ni Rashid Simai Msaraka ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Suzan Peter Kunambi anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A”, Hamida Mussa Khamis anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B”, Sadifa Juma Khamis anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “A”, Aboud Hassan Mwinyi anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B”.

Wengine ni Rashid Makame Shamsi anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kusini, Marina Joel Thomas anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati, Mgeni Khatib Yahya anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete, CDR Mohammed Mussa Seif ambaye anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni, Abdallah Rashid Ali anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake na Issa Juma Ali ambaye bado uteuzi wake unaendelea katika Wilaya ya Mkoani.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kutiwa saini na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Zanzibar Hassan Khatib Hassan Wakuu hao wapya wa Wilaya wataapishwa siku ya Jumaatatu ya terehe 04 Januari, 2021 saa 10 jioni.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.