Habari za Punde

WAZIRI MHAGAMA AMEKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MENEJIMENTI YA OFISI YA WAZIRI MKUU – KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akiongoza kikao cha Menejimenti kilichofanyika hii leo Januari 16, 2020 katika Ukumbi wa Mkutano uliopo Ofisi ya Waziri Mkuu, Ngome Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Patrobas Katambi (kulia) ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu), Mhe. Ummy Nderiananga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiongoza kikao hicho alipokutana na Menejimenti kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Ofisi hiyo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ndg. Andrew Massawe (kulia aliyesimama) akitoa taarifa kwa Waziri Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Mawaziri anayeshughulikia (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Patrobas Katambi (kushoto) na Mhe. Ummy Nderiananga anayeshughulikia (Wenye Ulemavu) wakati wa kikao kazi hicho.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.