Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amekutana na Kuzungumza na Ujumbe wa Kampuni ya Eliya Food Overseas limited ya Dubai.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Kampuni ya Eliya Food Overseas Limited kutoka Nchini Dubai, walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Kampuni ya Eliya Food Overseas Limited kutoka Nchini Dubai, ukiongozwa na Bw. Shabbir Virjee (kulia kwa Rais) walipofika Ikulu kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Ujumbe wa Kampuni ya Eliya Food Overseas Limited kutoka Nchini Dubai, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar

Rais Dk. Mwinyi alikutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa wawekezaji wa Kampuni ya “Eliya Food Overseas Limited” kutoka Dubai ukiongozwa na Bwana Shabbir Virjee ambao wameonesha nia na kueleza utayari wao wa kuekeza viwanda vya matunda, mbogamboga pamoja na viwanda vya uvuvi sambamba na kuonesha nia ya kusaidia wafanyabiashara wa soko la Darajani kwa kujenga sehemu maalum ya kuhifadhia bidhaa zao zikiwemo mboga mboga, samaki na bidhaa nyenginezo ili zisiharibike.

Rais Dk. Mwinyi aliueleza ujumbe huo wa wawekezaji wa Kampuni ya “Eliya Food Overseas Limited” kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari na imeshajipanga vyema kuwapokea wawekezaji wenye lengo la kuekeza Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuwawekea mazingira mazuri ya uwekezaji.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.