Habari za Punde

Waziri Gwajima Kuzikabili NGOs Korofi.

Na Mwandishi Wetu Dodoma

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima amesema Serikali haitavulia kuona Mashirika Yasiyo ya Kiseikali yafanya kazi bila kufuata sheria.

Dkt. Gwajima amesema hayo Bungeni Jjijini Dodoma wakati kuwasilisha Hotuba ya Mwelekeo wa Mapato na Matumizi ya Wizawa hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Amesema Serikali itaendelea kuimarisha ufuatiliaji na uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili yatoe mchango Chanya wa Ujenzi wa Taifa na hivyo kunufaisha Jamii.

Amesema pamoja na jitihada zinazoendelea kufuatilia na kuratibu shughuli za Mashirika hayo, Serikali itahakikisha jitihada zaidi inaongeza kukomesha Mashirika yasiyotimiza masharti.

" Sitokubali kuona Shirika lolote lisilo la Kiserikali kuona linafanya kazi bila kusajiliwa kwa mujibu wa Sheria sitovumilia hili litokee jisajilini mfanye kazi kwa utaratibu” alisema Waziri Gwajima.

Amesema shilingi milioni 585.5 zimetengwa  kwa aliji ufuatiliaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 1,000 Tanzania Bara.

Waziri Gwajima pia amezungumzia umuhimu wa kukuza Uzalendo wananchi na ari ya kujitolea kujiletea Maendeleo yao kwa kutumia rasrimali zinazowazunguka ambapo ushungi milioni 350.7 zimetengwa kufanikisha azma hiyo.

  Aidha amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kujifunza na kujifunzia na kuhakikisha wanawake wamepata  nafasi zaidi za uongozi na maamuzi.

Akizungumzia umuhimu wa makundi maalum katika Jamii wakiwemo watoto, wazee na wenye ulemavu, Mhe. Gwajima amesema Serikali itaaendelea kuboresha huduma za Ustawi wa Jamii, kuboresha huduma kwa Wazee, kufuatilia na kuimarisha uanzishaji wa vituo vya kulelea watoto wadogo na kuboresha huduma za usuluhishi wa migogoro ya ndoa na familia.

"Niseme jumla ya Shilingi bilioni 12.4 zimetengwa kwa ajili hiyo ikiwemo kukarabati majengo na miundombinu katika makazi 10 ya wazee ili kuwezesha kuwa na amzingira mazuri ya kulea wazee na wasiojiweza” alisema Waziri Gwajima.


Waziri Gwajima amesisitiza kuwa Wizara itaendelea kuratibu kampeni mbalimbali za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Jumla ya Shilingi milioni 791 zimetengwa kwa ajili ya kuratibu kampeni za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Wakichangia katika Hotuba huyo ya Bajeti baadhi ya Wabunge wamesema pamoja na jitihada za Serikali kukabiliana na vitendo vya Ulatili dhidi ya wanawake na Watoto vitendo kama ukeketaji bado vinaendelea katika maeneo kadhaa nchini.


Mbunge wa Viti maalum Grace Tendega amesema huduma kwa Wazee ikiwemo huduma rati kwa wote ziboreshwe ili kuboresha maisha kwa wote.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.