Habari za Punde

Uongozi wa Moto Small Simba Sport Club Wakutana na Rais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Mwinyi Ikulu Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Uongozi wa Timu ya Small Simba Sport Club alipowasili katika ukumbi wa mkutano Ikulu Jijini Zanzibar leo 8/6/2021.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Uongozi wa Timu ya Small Simba Sport Club, walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Small Simba Sport Club Ndg. Suleiman Mahmoud Jabir, akizungumza na kuwasilisha salamu zao klabu yao, wakati wa mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar na(kulia kwa Rais) Mwenyekiti wa Klabu ya Small Simba Sport Club mchezaji wa zamani wa timu hiyo Khamis Suleiman Mpemba
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa mpango kazi  wa Mradi wa Kituo cha michezo cha kilabu ya Small Simba Sport Club Zanzibar na Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Ndg. Suleiman Mahmoud Jabir, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa picha ya Kikosi cha Timu ya Small Simba Sport Club na Mtendaji Mkuu wa Timu hiyo Ndg. Suleiman Mahmoud Jabir baada ya kumaliza mazungomzo yake na Uongozi wa timu hiyo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Jezi ya Kilabu ya Small Simba Sport Club na Mtendaji Mkuu wa timu hiyo Ndg. Suleiman Mahmoud Jabir, baada ya kumaliza mazungumzo yake na Uongozi wa timu hiyo ulipofika Ikulu kwa mazungumzo 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuagana na Uongozi wa Timu ya Small Simba Sport Club, walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Timu ya Small Simba Sport Club, baada ya kumaliza mazungumzo na Uongozi wa timu hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.